MEYA ELIAS MASUMBUKO AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI CHANZO CHA MAJI MTO KIDALU
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MEYA wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ameongoza zoezi la upandaji Miti katika Chanzo cha Maji Mto Kidalu,ili kukitunza chanzo hicho pamoja utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Zoezi hilo la upandaji Miti limefanyika leo Desemba 27, 2023 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, pamoja na waandishi wa habari wakiongozwa na Mwenyekiti wao Greyson Kakuru ambaye pia ni Mwandishi wa habari kutoka Shirika la utangazaji Tanzania TBC.
Meya Masumbuko akizungumza katika zoezi hilo la upandaji Miti, amelipongeza Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuratibu upandaji huo Miti na kushirikisha viongozi, ili kuendelea kumuunga Mkono Rais Samia na Makamu wake Dk. Philip Mpango, ambao wamekuwa waumini wazuri wa utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Natoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga waendele kuzitumia mvua ambazo zinaendelea kunyesha kwa kupanda Miti kwa wingi, ili kuyatunza mazingira na hata kuupendezesha Mji wetu wa Shinyanga na kuwa wa kijani,”amesema Masumbuko.
“Mbali na utunzaji Mazingira Miti inafaida nyingi sana na hata kuwa na ulinzi wa nyumba zetu ili zisiezuliwe na upepo,mfano hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya nyumba zimeezuliwa na upepo hapa Shinyanga kutokana na ukosefu wa miti, naombeni tupande Miti kwa wingi,”ameongeza.
Naye Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga, amesema zoezi hilo la upandaji miti ni endelevu, na kwamba ndani ya mwaka huu wameshapanda Jumla ya Miti zaidi ya Milioni 1.2 na kwamba maagizo ya Serikali ni kupanda Miti Milioni 1.5 kwa kila Halmashauri ndani ya mwaka mzima.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga waendelee kupanda Miti kwa wingi ya matunda na kivuli, na wale ambao wanahitaji Miti wanaweza kufika katika Ofisi yake ili wapewe Miti bure.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Greyson Kakuru,ambaye pia ni Mwandishi wa habari (TBC)amewashukuru viongozi pamoja na wananchi, kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo la upandaji miti, pamoja na kumuunga Mkono Rais Samia na Makamu wake Dk. Mpango kuendelea kutunza Mazingira ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti katika Chanzo cha Maji Mto wa Kidalu.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji Miti.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akipanda Mti.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akipanda Mti.
Diwani wa Ibanzamata Ezekiel Sabo akipanda Mti.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
Muonekano wa Mto Kidalu.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akifyeka Majani kwa ajili ya usafi wa Mazingira.
Zoezi la Usafi wa Mazingira na uchimbaji wa mashimo kwa ajili ya kupanda Miti likiendelea.
Zoezi la Usafi wa Mazingira likiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa katika zoezi hilo la upandaji Miti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464