ASKOFU SANGU ALAANI UTOAJI MIMBA
-Watoto ni zawadi,baraka kutoka kwa Mungu
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amelaani tabia ya utoaji mimba kwa kuwaua watoto wasio na hatia ambao bado hawajazaliwa, kwa tamaa ya kuendekeza starehe za dunia.
Amebainisha hayo leo Desemba 28, 2023 kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya watoto mashahidi ambao waliuawa kikatili na Mfalme Herode siku chache baada ya kuzaliwa Kristo, Ibada iliyofanyika Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga iliyoambatana na utoaji wa Sakramenti ya Kipaimara.
Amesema watoto ni zawadi na baraka kutoka kwa Mungu, hivyo kitendo hicho cha utoaji mimba kinapaswa kukemewa.
“Tusiwaue watoto ambao bado hawajazaliwa sababu ya kuendekeza starehe za dunia, tukaemee hiki kitendo watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu,”amesema Askofu Sangu.
“Kila Mtu anawajibu wa kulinda haki za watoto kabla ya kuzaliwa na hata baada ya kuzaliwa, watoto ni zawadi ya Mungu tuwalee na kuwatunza na tuwafaundishe kumjua Mungu,”ameongeza.
Katika hatua nyingine Askofu Sangu, ameiomba Serikali kupiga Marufuku Vituo vya kulea watoto “Baby Care” ambavyo vimekuwa ni moja ya chanzo cha Mmomonyoko wa maadili kwa watoto na kufundishwa mambo ya hovyo ikiwamo mapenzi ya Jinsia Moja.
Amesema Vituo hivyo vya kulea watoto “Baby Care” havifai kuwepo bali kila mzazi anapaswa kumlea mtoto wake katika maadili mema, na siyo kuwa bize na maisha na kwenda kulelewa na watu wengine na kufundishwa mambo ya hovyo .
“Mtoto wa kuanzia mwaka Mmoja hadi Mitano anapaswa kuwa karibu na wazazi, na siyo kumpeleka kwenye ‘Baby Care’ ambapo wanafundishwa mambo ya hovyo ikiwamo mapenzi ya jinsia moja, tunaomba Serikali ipige marufuku vituo hivi,”amesema Askofu Sangu.
“Kanisa Katoliki tunapinga kabisa mapenzi ya Jinsia Moja, hata Tamaduni zetu za Kiafrika zinapinga tamaduni hizi za kigeni na huu ni Ushetani kabisa,”ameongeza Askofu Sangu.
Nao baadhi ya wazazi wamesema suala la kupeleka watoto kwenye vituo vya kulelea watoto “Baby Care” linatokana na kuwa bize na maisha pamoja na kukosa mtu wa kuwachia nyumbani, ikiwa wafanyakazi wa siku hizi nao wamekuwa siyo wa kuaminika ambapo huawafanyia watoto ukatili.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI👇👇
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akizungumza kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya watoto mashahidi.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Watoto wakiwa kwenye Misa.
Watoto wakiwa kwenye Misa.
Watoto wakiwa kwenye Misa.
Askofu Sangu akiongoza maandamano ya kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464