RC MNDEME AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UTAWALA MSALALA,AWATAKA WATUMISHI WABORESHE UTENDAJI KAZI KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI
Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameweka jiwe la Msingi katika Jengo la Utawala Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, huku akiupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa ujenzi wa ofisi hiyo, na kuwataka watumishi wabadilike wawe wapya kama lilivyo Jengo lao jipya la utawala na kwamba waboreshe zaidi utendaji kazi kwa kutoa huduma kwà wananchi.
RC Mndeme amebainisha hayo leo mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la utawala linalogharimu zaidi ya Bil. 4 ikiwa ni ishara ya kudunguliwa rasmi na kutoa huduma kwa wananchi na kuwapongeza kwa samani za ofisi zilivyo nzuri na bora zaidi kuliko za nje ya nchi, samani zilizonunuliwa hapa wilaya ya kahama na kuelekeza halmasbauri nyingine hasa ya Manispaa ya shinyanga na shinyanga DC kuja kujifunza Msalala.
"Nawapongeza sana uongozi wa Halmashauri ya Msalala kwa kusimamia na kujenga jengo la watumishi na kuamua kununua samani za ofisi hapa hapa wilaya ya kahama zenye thamani zaidi ya zile za nje ya nchi, na pia nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania tupenda vyetu", amesema RC Mndeme.
Aidha, RC Mndeme amewaeleza watumishi hawa kuwa, kuwa jengo jipya ni hatua moja lakini kupanga mipango yenye tija kwa wananchi ndiyo jambo muhimu zaidi ili wananchi waweze kuhisi mabadiliko haya muhimu kwao ukizingatia wan ndiyo tunawahudumia na ndiyo maelekezo yq Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia wananchi.
Awali akitoa salamu za Halmashauri kwa RC Mndeme mkurugenzi wa halmashauri ya msalala Ndg. Hamis Katimba alimshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaptia fedha hizi ambazo zimewezesha wao kutoka katika kufanya kazi kwenye mazingira magumu ya msongamano ofisini na sasa wanafanya kazi vizuri sana kwa ubora wa huduma unaotakiwa.
Katimba alisema wamebakiza upande mmoja kuhitimisha ujenzi kamili wa jengo ambapo gharama zake ni zaidi ya Bilioni moja na hivyo kukamilisha gharama ya zaidi Bilioni 4 kwa jengo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464