RC MNDEME AWASHAURI WANANCHI WALIO KWENYE MPANGO WA REA KUUNGANISHA UMEME
Na. KAHAMA MC
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewashauri wananchi waliopo kwenye mpango wa kuunganishiwa umeme wa REA Mkoa wa Shinyanga kuuza walau kuku mmoja au wawili ili kupata Tzs. 27,000 kisha kulipia gharama za kuunganishiwa umeme wa REA.
RC Mndeme amewaeleza wananchi hao leo tarehe 13 Desemba, 2023 alipokuwa akiwasha umeme katika kijiji cha Kahanga kilichopo Manispaa ya Kahama kuwa gharama nyingine za nguzo na waya za kuingia kwenye nyumba husika ambapo awali mwananchi alikuwa akilipia zaidi yq Tzs. 500,000/ sasa zimeishalipiwa na Serikali.
Hivyo ni wajibu wa kila kila nyumba kuwa na Nishati ya Umeme kwani umeme ni uchumi na siyo starehe wala anasa.
"Ndugu zangu wananchi, serikali imeishagharamia gharama zote ambazo awali zilikuwa zinaongeza gharama kama bile nhuzo na waya na kufanya gharama kuzidi hata laki tano, kilichopo hivi sasa ni kulipia Tzs. 27,000 tu na kama huna uwezo kabisa basi uza angalau kuku mmoja au wawili hapo unapata pesa hiyo na chenji inabakia ili kila nuumba iwe na umeme kwani ni uchumi na siyo anasa tena", amesema RC Mndeme.
Awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Mhandisi Anthony Tarimo ambaye ndiye anayesimamia miradi ya REA Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa, mkandarasi amewasha nyumba 16 kati ya 26 kwa Manispaa ya Kahama na anatarajia kukamilisha ifikapo Desemba 31, 2023 ambapo atakuwa amevifikia vijiji 146 vya mkoa wa shinyanga.
RC Mndeme yupo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kuendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa hapa .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Ndg. Thomas Mnyonga alimpongeza sana mhe. Mndeme kwa namna ambavyo anamsakdia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo na hata leo amefika hapa Kahanga kuwasha umeme kwa niaba ya vijiji vingine 26 ambapo 16 tayari vimewekewa umeme.
Aidha ndg. Thomas amewataka wananchi wa kahama kujenga nyumba bora na za kisasa zaidi mqqnq serikali inaleta umeme, barabara na huduma nyingine muhimu karibu yao na haya ndiyo maelekezo ya mwenyekiti wa ccm Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwafikia wananchi kimaendeleo na kuwajali.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464