POLISI SHINYANGA WAMEWAKAMATA WANAWAKE RAIA WA BURUNDI TUHUMA WIZI WA SIMU
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limekamata vitu mbalimbali vya wizi zikiwamo simu 61 ambazo zimeelezwa kuibwa na Wanawake Watatu ambao ni Raia wa Burundi katika Minada Mbalimbali.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amebainisha hayo leo Decemba 20, 2023 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Misako na Doria ambayo wameifanya kwa muda wa kipindi cha kuanzia Novemba 30 hadi Decemba 19 mwaka huu.
Amesema katika msako huo wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya wizi zikiwamo simu hizo 61, huku wakikamata pia Pombe aina ya Moshi Lita 73, Mafuta ya Dizeli lita 260, Pikipiki 7, TV 4, vyuma vya kuchimba visima 9, Groli za Karasha 106, Bangi Misokoto 15, na Subwoofer 2.
Ametaja Vitu vingine kuwa ni Difu Moja ya Gari aina ya Toyota aina ya Hiace, Noti Bandia 9, ‘Pipe’ 11 za kunyonya Mafuta, Baiskeli Moja, Vipande vya Nondo 6, Keyboard Moja, ‘Chesses’ Moja ya Pikipiki, Spika 2, na Vifaa mbalimbali vya kupigia Ramli Chonganishi ambavyo ni Mikia 8 idhaniwayo kuwa niya Nyumbu, Kipande cha Simba.
“Jeshi la Polisi katika Msako na Doria ambayo tumeifanya kwa kipindi cha Novemba 30 hadi Decemba 19 mwaka huu, tumekamata vitu mbalimbali vya wizi na watuhumiwa tumewakamata kwa hatua zaidi za kisheria,”amesema Magomi.
Aidha, kwa upande wa Mafanikio ya Kesi za Mahakamani amesema Kesi 8 zimepata mafanikio ambapo Moja ya Ubakaji mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela, Kesi 2 za kujipatia Pes kwa njia ya udanganyifu washitakiwa wamehukumiwa kwenda Jela miezi 6 hadi miaka 3.
Ametaka Kesi nyingine kuwa Moja ya kuharibu Mali Mshitakiwa alihukumiwa Jela miezi 5, Kesi mbili za Pikipiki Washitakiwa walihukumiwa kwenda Jela miaka Miwili.
Katika hatua nyingine Kamanda amesema katika kudhibiti Ajali za usalama barabarani Jeshi hilo limefanikiwa kukamata Jumla ya Makosa mbalimbali 2,806 Kati ya hayo makosa 5 kwa kusababisha Ajali, kuendesha mwendokasi na matumizi mabaya ya barabara na Madereva kulipa faini.
“Hatua mbalimbali tunazoendelea kuzichukua katika kudhibiti Ajali za Barabarani pia kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga tumefanikiwa kutoa elimu kwa makundi yote yanayotumia barabara kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani na nina wasisitiza madereva kufuata sheria za barabarani na dereva atakaye vunja sharia atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema Magomi.
Pia amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili kuendelea kuimarisha usalama wa Mkoa wa Shinyanga, pamoja na wazazi kuwa makini na watoto wao kwa kufuatilia mienendo yao hasa katika msimu wa sikukuu za Christima na mwaka mpya.