RC MNDEME ARIDHISHWA UJENZI KITUO CHA POLISI ULOWA


RC MNDEME ARIDHISHWA UJENZI KITUO CHA POLISI ULOWA.

Na. Shinyanga RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina  Mndeme, amepongeza utekelezaji wa mradi wa ujenzi Kituo kidogo cha Polisi Ulowa kinachojengwa kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi, serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Pongezi hizi zimetolewa jana alipotembelea kukagua ujenzi huo wa Kituo cha Polisi ambacho kimetajwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa Kata ya Ulowa ambapo kwa sasa huduma ya Polisi inatolewa kutoka kwenye nyumba ya kupanga.
"Nakupongeza sana Mkuu wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi kwa kazi nzuri ya kutekeleza takwa la kisheria la kulinda wananchi na mali zao katika mkoa huu wa shinyanga ikiwemo na kata ya ulowa pamoja na kusimamia ujenzi wa kituo hiki cha polisi ulowa", amesema Mndeme.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho cha Polisi Mkuu wa Kituo cha Polisi Ushetu, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Chrisantus Kavishe amesema kuwa kituo hicho kinakwenda kuwa Mwarobaini wa kutatua matatizo yote na kukomesha uhalifu.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyinga ACP Janeth Magomi amesema wao kama Jeshi la polisi wamejipanga vema sana kulinda raia na mali zao kwakuwa ndiyo takwa la kisheria, na kwamba hakuna mhalifu atakayeweza kutishia amani wananchi mkoa wa Shinyanga.
Hayo yamejili baada ya kukithiri kwa matukio ya uhalifu kwenye Kata hiyo ya Ulowa, ambapo imeelezwa kuwa wahalifu walikuwa wakifika na kufanya matukio ya unyang'anyi jambo ambalo lilipelekea kupata hasara ya mali,pesa na kukosekana Amani kwa Wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464