WAATHIRIKA MVUA YA MAWE,UPEPO KIJIJI CHA IBANZA SHINYANGA WAMEPEWA MSAADA NA SERIKALI, NYUMBA ZILIZOANGUKA ZIMEFIKA 60
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WANANCHI wa Kijiji cha Ibanza Kata ya Mwamala wilayani Shinyanga, ambao walipata maafa ya mvua ya mawe na upepo na kusababisha nyumba zao kuanguka na kuharibu mashamba, wamepewa msaada na Serikali wilayani humo.
Misaada ambayo wamepewa ni Chakula, Matent pamoja na Mbegu za Mahindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo, amesema wametekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ambaye siku ya tukio Decemba 6, aliangiaza waathirika hao wapewe msaada wa haraka.
“Serikali tupo pamoja na waathirika hawa hadi pale maisha yao yatakaporudi kama zamani, na tunaendelea kuwapatia misaada mbalimbali, na leo tumeleta Mbegu za Mahindi Kilo 106,amesema Maduhu.
Nao baadhi ya Waathirika wa Mvua hiyo akiwamo Jilala Dutu wameishukuru Serikali kuwa pamoja nao kwa kuwapatia msaada huo, huku wakiendelea kujipanga kujenga nyumba nyingine ambazo ni imara.
Diwani wa Kata ya Mwamala Hamis Masanja, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwa pamoja nao tangu siku ya tukio pamoja na kuendelea kupeleka misaada kwa waathirika.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ibanza Hassani Barabara, amesema kwa Tathimini ambayo wameifanya upya, nyumba ambazo zimeanguka zimefika 60 kutoka 51, huku Mashamba ambayo yameathirika yamefikia Hekali 85 kutoka Hekali 10.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, (kulia)akimkabidhi Mbegu za Mahindi Diwani wa Mwamala Hamis Masanja kwa ajili ya wananchi ambao Mashamba yao yaliathiriwa na Mvua ya Mawe na upepo.
Zoezi la Makabidhiano ya Mbegu za Mahindi likiendelea.
Zoezi la Makabidhiano ya Mbegu za Mahindi likiendelea.
Muonekano wa Mbegu za Mahindi.
Waathirika wa Mvua wakiwa na Mbegu za Mahindi.
Muonekano wa Mbegu za Mahindi.
Waathirika wa Mvua wakiwa kwenye Tent.
Bibi ambaye alivunjika Mguu katika Maafa ya Mvua akiwa ametoka Hospitali
Mbegu za Mahindi.