RC MNDEME AIPONGEZA MSALALA KWA UJENZI WA SEKONDARI YA KAKOLA, BULYANHULU S/M NA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA ZA SERIKALI


RC MNDEME AIPONGEZA MSALALA KWA UJENZI WA SEKONDARI YA KAKOLA, BULYANHULU S/M NA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA ZA SERIKALI.

Na. Ushetu - Shinyanga.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa ujenzi bora wa shule ya sekondari Kakola iliyogharimu zaidi ya Tzs. Mil. 603 pamoja na shule ya msingi Bulyanhulu iliyogharimu Mil 561 huku akiridhishwa sana kwa namna walivyosimamia matumizi ya fedha za serikali.


RC Mndeme ameyasema hayo jana alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya ushetu huku akimpongeza sana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Mibako Mabubu, waheshimiwa madiwani wote, Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa fedha za serikali zinazotolewa na serikali ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi wa msalala na shinyanga kwa ujumla.

"Kwa dhati ya moyo wangu, niwapongeze sana Msalala kwa kazi nzuri ya ujenzi wa shule hizi mbili zenye kuvutia na zenye kuonesha uhalisia wa thamani ya fedha, huu ndiyo usimamizi mzuri wa fedha za serikali unaotakiwa,
", amesema RC Mndeme.

Kando na pongezi hizo RC Mndeme amesema kuwa, uwepo wa wawekezaji nchini unatokana na mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji yaliyowekwa na Rais Skr. Samia Suluhu Hassan na ndiyo sababu mnaona wapo na wataendelea kuweko Barrick hapa Msalala.

Ziara ya RC Mndeme imejumuisha ukaguzi na uwekaji wa mawe ya msingi katika mbalimbali Msalala ambapo ameweka jiwe la msingi katika jengo la watumishi wa msalala, usambazaji wa umeme wa REA kijiji cha Bunva.

Miradi mingine ni ujenzi wa jengo la wodi maalum la huduma za haraka (Fast Truck), kisha alikagua sekondari ya wasichana Bulyanhulu inayojengwa na Barrick fedha za mrejesho wa faida kwa umma utokanao na mapato ya mgodi na mwisho akahitimisha na shule.

Leo tarehe 13 RC Mndeme ataendelea na ziara yake katika Manispaa ya Kahama ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia atatembelea na kukagua kituo uwezeshaji Mondo, kutembelea na kukagua kituo cha uwezeshaji Mwendakulima na kuwasha umeme kijiji cha Kahanga kata ya Wendele hapa Kahama.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464