Wilaya ya Kishapu imeungana na watanzania wote nchini kusheherekea miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania bara katika ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Kishapu maadhimisho haya yamesheheneshwa na kauli mbiu ya mwaka isemayo UMOJA NA "MSHIKAMANO NI CHACHU YA MAENDELEO YA TAIFA LETU"
Kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Dkt. Sabinu Chaula amewapongeza wananchi na watumishi wa ngazi mbalimbali chama na Serikali na viongozi wa dini kwa namna walivyojitokeza kuitikia wito wa kusheherekea miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania.
Aidha Dkt Sabinu ameeleza jinsi ambavyo Serikali imefanya kazi kubwa kwa Halmashauri ikiwa ni Pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokamilika na inayoendelea kujengwa katika kada mbalimbali hususani, Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara, maji, umeme.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Kishapu Bi Fatma H. Mohamed ambaye alikuwa mgeni rasmi, katika maadhimisho hayo amesema tangu kupata uhuru Kishapu inajivunia kwa kuwa na mafanikio yenye tija hasa katika kipindi cha awamu ya Sita katika sekta mbalimbali za kilimo, viwanda,Elimu,miundo mbinu Afya maji.
jambo ambalo awali haikuwa rahisi katika maeneo mengi
"Tunamshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutufikisha salama katika siku ya leo, Tangu kupata uhuru Kishapu tunajivunia mafanikio mengi makubwa nikijikita hasa katika miaka Miwili ya awamu ya Sita Wilaya ya Kishapu imekuwa na makubwa katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Umeme bila kusahau uzalendo ambao ndiyo nguzo kubwa ta Mshikamano wetu" amesema Fatma
Vile vile Katibu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Peter Mashenji amesema kizazi cha sasa nivyema kikapatiwa elimu ili kufamu tulikotoka tulipo na tunapokwenda hii itasaidia Vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao na kufamu kwa undani mafanikio ambayo yanatekelezwa na serikali
Kwa upande wake Meja James Sana amekiri kuwepo kwa mabadiliko makubwa baada ya Uhuru ikiwemo uboreshaji wa haki za kila Mtanzani kupa elimu tofauti na hapo awali Elimu walikiwa wakipata watoto wa watemi na sivinginevyo pia amepongeza Sana awamu ya sita jinsi inavyojipambanua katika utekeleza wa miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa
Naye Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson ameipongeza Sana serikali kwa kuona inafaa maadhimisho haya kufanyika katika kata yake sambamba na hilo amepongeza mafanikio makubwa yanayofanywa na Serikali
" Ninawasukuru sana kwa kuona kataya Kishapu inafaa kwa maadhimisho haya pia naomba nijikite kuipongeza serikali kwa mafanikio makubwa ambayo inayatejeleza hasa kwa miaka miwili ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt, Samia katika wilayetu tumepiga kasi kubwa San katika nyanja mbalimbali kama vile Elimu, Afya, barabara, umeme na Maji" amesema Joel
Hata hivyo maadhimisho hayo yaliambatana na upandaji wa miti katika soko la wajasiliamali shule ya msingi igaga ambapo Wilaya imepanda zaidi ya miti 900 ikitekeleza Maagizo ya Serikali ya utunzaji wa Mazingira.
Aidha katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed amewataka Wananchi wa Kishapu kuzitumia Mvua hizi katika upandaji miti ili ziweze kuleta tija katika ukuaji wa miti pia amewataka wajijengee dhana ya kupanda miti majumbani na baadhi ya maeneo yao ya wazi.