BOT KUWAKWAMUA WAATHIRIKA MIKOPO UMIZA,KAUSHA DAMU


BOT kuwakwamua waathirika mikopo umiza, kausha damu

DAR ES SALAAM: BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imezindua rasmi mtaala wa wakufunzi wa elimu ya fedha nje ya mfumo rasmi ambapo wananchi watapata elimu ya matumizi sahihi ya fedha ikiwemo akiba ili kuepuka mikopo umiza na kausha damu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam, Gavana wa BOT, Emanuel Tutuba amesema mtaala huo utakuwa na fursa nzuri ya kuona matokeo chanya katika shughuli mbalimbali kwenye upatikanaji wa mikopo, matumizi na hata urejeshaji kwa makundi ya wajasiriamali, wakulima, wavuvi na wengine.

Amesema wanafahamu changamoto ya mikopo chechefu inayotokana na kutokuwa elimu stahiki ya utaalamu wa fedha hivyo wanaendelee kushirikia wote ili kutoa elimu.

“Utakuta mtu anaweza kukopa ili kufanya shughuli ambazo haziwezi kurejesha ukopo huo sio mzuri hii yote ni elimu duni ya fedha na wengine wanamipango mingi akipata fedha ni mwepesi kubadili vipaumbele kitu ambacho sio sahihi,” amesema Gavana.

Tutuba amesema kuwa kila mmoja ana uwezo wa kushika fedha shida inakuja namna ya kuzitawala ambapo watu wanakuwa na matumizi mabaya hivyo mtaala huo utawawezesha kutoa elimu ili iwafikie wananchi.
“Watu tunawasisitiza kabla ya kuchukua mikopo lazima awe amefahamu masharti kwamba unapoingia mkataba lazima wote mridhie tunasisitiza mikopo yote watu lazima wakubaliane na mtu akiambiwa riba afahamu ni ya mwaka,mwezi,siku maana kuna wengine wanachukua mkopo anazidisha wiki mbili atarejesha na ataambiwa kuwa atalipa faini.

Wadau watatoa elimu hiyo ya fedha mwaka 2024 nchi nzima ambapo wakufunzi mbalimbali wakiwemo wale wenye elimu ya fedha,wanaotoka vyuo mbalimbali,halmashauri,taaluma zingine watapata mafunzo ya wiki mbili na kupewa vyeti.

Soma hapa zaidi chanzo habari leo

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464