DC KAHAMA - KASI YA ULIPAJI KODI NDIYO UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ISIFANYIKE BIASHARA YA MAGENDO


Kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi mkoa wa kikodi Kahama.

Na  Kareny Masasy,Kahama

MKUU wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita  amesema  kodi inamchango mkubwa kwa maendeleo na kasi kubwa ya ulipaji kodi ndiyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo  hivyo  baadhi ya wafanyabiashara waache kutisha wateja na kuendesha biashara za magendo.

Mhita amesema hayo jana tarehe 2/Desemba ,2023  alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha shukrani kwa mlipakodi  mkoa wa kikodi Kahama  huku akiwatunukiwa vyeti baadhi ya wafanyabishara wakubwa na wadogo  kwa jitihada za ulipaji kodi kwa ufanisi.

Mhita amesema ulipaji kwa kodi kwa hiari unaonyesha jitihada za kuunga mkono serikali kufanikisha miradi ya maendeleo  kama ujengaji wa miundombinu ya barabara,shule, hospitali nawapongeza  TRA Kahama  namna ya  usimamizi mzuri wa ulipaji kodi.

Kauli mbiu “Kodi yetu maendeleo yetu tuwajibike”  ili kuwa na kumbukumbu sahihi za baishara yako  lazima ujue   kodi inayotozwa hivyo   utunze kumbukumbu  na hapo utalipa  vizuri kuliko usiotunza  kumbukumbu”amesema  Mhita.

Mhita  amewakumbusha wafanyabiashara  matumizi ya utumiaji wa mashine za  kielektroniki (EFD)  ikiwa  lazima  kuendana na matumzi ya kidijitali  sambamba na muuzaji kutoa risiti kwa wateja na kuondoa dhana potofu ya kueleza wanaibiwa ambapo   ushauri watumie risiti.

Naibu mkurugenzi wa  fedha kutoka  TRA makao makuu Anna Mdeme  amesema Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  ametoa kipaumbele  na kufanya mapinduzi makubwa ya  usimamizi wa kodi kwa kutatua upungufu wa watumishi na kuridhia  uboreshaji wa mamlaka hivyo wameimarika kwa kiasi kikubwa nakutambua mchango mkubwa wa walipa kodi.

"Mwaka wa fedha  2022/2023  mamlaka ilifanikiwa kukusanya sh Trioni  24.11 sawa na ufanisi wa asilimia 97.4 ya makusanyo ya jumla ya  lengo  na ikiwa ni  ongezeko la asilimia 8.2  ikilinganishwa na makusanyo ya  mwaka 2021/2022 hivyo wanashukuru walipa kodi kwa dhana ya kauli moja na walipa kodi”amesema Mdeme.

Ukusanyaji wa mapato ni shughuli endelevu  inahitaji kuimarika siku zote  Mwaka  2023/2024 kuanzia  Julai   mamlaka  ina lengo  la kukusanya sh tironi 28. 4 ikiwa  Sh Trioni   27.8 Tanzania bara na  Bilioni 520.6  Tanzania visiwani   mafanikio yameridhisha  mpaka sasa .

Mdeme amesema  kuanzia   mwaka 2022/2023   Julai  hadi Septemba robo ya kwanza  ya mwaka wa fedha wamekusanya   sh Trioni 6.58 sawa na ufanisi asilimia 97.53   makusanyo hayo ni ongezeko  kubwa la asilimia 11.05  ila mwaka uliopita walikuwa na ongezeko la asilimia 8.

Mdeme amewashauri  wafanyabiashara waache kuficha taarifa zao ili kuweza kukusanya mapato,hivyo huduma bora zenye uwajibikaji ndiyo msingi bora wa kulipa kodi na mmamlaka imeeleza kutoa elimu zaidi ili kuleta uwajibikaji kwa walipa kodi.

Kaimu meneja kutoka (TRA)  mkoa wa kikodi Kahama Wisaka  Kamwamu amesema mapindizi kwa ulipaji kodi umeleta ufanisi mkubwa kwa kila siku kwa wafanyabiashara na  wafanyakazi.

“Ikiwa mkoa wa kikodi Kahama umefanikiwa  kukusanya kodi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Julai hadi Novemba  mwaka wa fedha 2023/2024  kwa kukusanya sh Bilioni 6.59  sawa na ufanisi wa asilimia 125 ambapo malengo ya makusanyo yalikuwa ni sh Bilioni 7.2”amesema Kamwam.

Mwenyekiti wa  chemba ya wafanyabishara,viwanda na kilimo (TCCIA ) wilaya ya Kahama Charles Machali amesema  kutunukiwa  vyeti wafanyabiashara na kuongezeka  mapato  ni jitihada zilizofanywa  kwa ushirikiano kwani zamani TRA ilikuwa adui sasa ni marafiki.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita katikati ni mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara,viwanda na kilimo Charles Machali  wakimpongeza  mkurugenzi wa shule za Anderleck na Rocken Hill  akipokea cheti cha pongezi kutoka TRA


Mfanyabiashara akipongezwa kwa kupewa cheti cha ulipaji kodi kwa ufanisi kutoka TRA.

viongozi wa  TRA  akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita pamoja na mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara, viwanda na kilimo Charles Machali wakisubiri kutoa tuzo na vyeti

Kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi mkoa wa kikodi Kahama



Picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya kielele cha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi




Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara,viwanda na kilimo (TCCIA) wilaya ya Kahama Charles Machali akitoa neno la shukrani kwa TRA
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464