KAMPUNI YA CANON GENERAL SUPPLIES YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA 32 WA TUKIO LA MAFURIKO KATA YA KIZUMBI


Kampuni ya Canon General Supplies ya mkoani Shinyanga ikitoa msaada kwa waathirika 32 wa tukio la mafuriko katika kata ya Kizumbi

Na Shaban Alley, Shinyanga press blog

Waathirika 32 wa tukio la mafuriko katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga wanahitaji misaada ya Kibinadamu ikiwemo Vyakula.

Diwani wa Kata hiyo Lubeni Kitinya amesema hayo wakati alipokuwa akipokea misaada mbalimbali kutoka katika kampuni ya Canon General Supplies ya mkoani Shinyanga amesema kuna kipindi viongozi wanalazimika kuchangishana fedha kwa ajili ya kuwahudumia waathirika hao waliohifadhiwa kwenye Shule ya Msingi Nhelegani.

Kitinya ameishukuru kampuni ya Canon ambayo imekuwa ya kwanza kutoa misaada hiyo na kutoa wito kwa wasamalia wema wengine ikiwemo Serikali kuwasaidia waathirika hao.

Kwa upande wake meneja wa Kampuni ya Canon Lazaro Saimon amesema wameguswa na tukio hilo la mafuriko lililotokea katika kata ya Kizumbi ambapo kampuni yao imewekeza.

Saimon ametoa wito kwa makampuni mengine na wasamalia wema kujitokeza kuwasaidia waathirika hao.
Waathirika wa tukio la mafuriko katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupewa msaada
Waathirika wa tukio la mafuriko katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupewa msaada.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464