Suzy Luhende Shinyanga press blog
Mbunge wa jimbo la Shinyanga ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi ameitaka Jumuiya ya vijana Wilaya ya Shinyanga mjini kuacha kujiunga na vikundi visivyokuwa na maadili mema vinavyo tumia madawa ya kulevya badala yake wakemee tabia hizo na waweze kujitunza.
Hayo ameyasema leo kwenye baraza la UVCCM wilaya ya Shinyanga ambapo amewataka vijana wajitambue na wajitunze ili kwa badae waweze kuwa viongozi wazuri na kujibidisha kufanya kazi ili kujiongezea kipato.
Amesema mtaji namba moja wa kijana ni kuwa na afya njema,kwani ukijitunza na kuwa na afya njema utafanya kazi na kujipatia kipato, lakini afya yako ikiwa lege lege haina afya huwezi ukajumuikana watu huwezi ukafanya kazi,hivyo ni vizuri wajilinde.
"Niwaombe vijana wangu mjitambue muwe na subira mjitambue na kujua na mjijue kuwa nyinyi ni vijana mkijitambua hamuwezi kukimbilia kwenye madawa ya kulevya na bangi, hivyo niwaombe muwe na uzalendo, msimame vizuri kwenye elimu zenu au kwenye kazi zenu,"amesema Katambi.
" Tukilinde chama chetu kwa gharama yeyote tusikubali kurudi nyuma tufanye kazi kwa ushirikiano na mnatakiwa kuwa na ndoto na malengo, shabaha namakusudio na kuwana elimu dini,kwani Mungu ametupa talanta kila mmoja hivyo tuzitumie talanta zetu,"amesema Katambi
"Mmesema mna miradi 23 vikiwemo vyumba vya vibanda 23 vya kudumu na ukiwemo ujenzi wa nyumba ya katibu nitashirikiana nanyi kwa kutoa mchango wangu, sitawaangusha nitaendelea kufanya mimi kama mbunge nitatafuta mbalimbaliili kuhakikishatunashirikiana katika kuumaridha miradi hii na kuhakikisha inafanya kazi,"amesema
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Ally Majeshi amewataka washirikiane katika kukijenga chama kwa kushirikiana , kwani jumuiya ya vijana inategemewa sana katika kupambana na kukiimalisha chama, hivyo wasiwe chanzo cha migogoro .
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula amewataka vijana kusimamia chama kwa nguvu zote ili kuhakikisha mwaka 2025 kinapata ushindi mkubwa wa kishindo, na kila kijana ahakikishe analipa ada na kuweza kuwaeleza wananchi kazi zinazosimamiwa na chama chama cha mapinduzi CCM.
"Kila kijana afanye wajibu wake maagizo haya tunayowapa mhakikishe mnayafanyia kazi, ili siku tutakayokutana mlete mrejesho wa kazi yenu, niwaombe sana myazingatie haya yote, pia simamieni chama cha mapinduzi huku mkifanya kazi kwa ushirikiano katika kukijenga chama chetu,"amesema Katalambula.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Jonathan Madete amewataka vijana waendelee kupambana ili kuhakikisha kuna usalama katika chama, na kuhakikisha wanalipa ada kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kushirikiana kwa pamoja kufanya kazi za chama pale wanapohitajika.
"Vijana ndiyo chachu ya maendeleo hivyo mnatakiwa kuwa chachu mjitume katika kufanya kazi zenu ili kujiongezea kipato pia mjitume katika kufanya kazi za chama ili kuhakiksha chama cha mapinduzi kinaendelea kuwa na nguvu na msimamie miradi mbalimbali iliyopo katika kata zenu, bila kusahau kuhamasisha vijana kujisajili na kulipa ada,"amesema Madete.
Katika kikao hicho cha baraza la vijana alihudhulia katibu mkuu wizara ya maji prof Jamal Katundu ambaye alikuwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kushughulikia maji ambaye amewataka vijana kusimama imara na kujua wajibu wa kazi zao.
"Mimi nipo hapa Shinyanga kwa ajili ya kufanya wajibu wangu, hivyo niliposikia mpo hapa na rafiki yangu Naibu waziri
ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi nimeona nije niwasalimie na nimefika hapa kwa ajili ya kufatilia changamoto za maji, hivyo mkipata changamoto ya maji msisite kuniambia nipo kwa ajili yenu nafanya kazi usiku na mchana,"amesema Katundu.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM Shinyanga mjini Jonathan Madete akizungumza kwenye kikao cha baraza
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akizungumza kwenye kikao cha baraza la vijana.
Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Ally Majeshi akizungumza kwenye baraza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya vijana CCM Piter Frank akizungumza kwenye baraza hilo
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akizungumza kwenye kikao cha baraza la vijana.
Katibu mkuu wizara ya maji prof Jamal Katundu akisaini baada ya kuingia kwenye baraza la vijana kwa ajili ya kuwasalimia
Katibu mkuu wizara ya maji prof. Jamal Katundu akizungumza kwenye baraza la vijana wa CCM wilaya ya Shinyanga.
Viongozi wa CCM na jumuiya ya vijana akiwemo mbunge wajimbo la Shinyanga wakiwa na Katibu mkuu wizara ya maji prof. Jamal Katundu
Viongozi wa Jumuiya ya vijana wilaya ya Shinyanga mjini
Mbunge wa jimbo la Shinyanga ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akimkaribisha Katibu mkuu wizara ya maji prof. Jamal Katundu kwenye kikao cha baraza la vijana CCM wilaya.
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya
Viongozi wa CCM na jumuiya ya vijana akiwemo mbunge wa jimbo la Shinyanga wakiwa wakiimba baada ya mbunge wa jimbo hilo kuwasili kwenye kikao hicho
Wajumbe wa baraza lavijana UVCCM wilaya ya Shinyanga wakifurahia jambo
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi akizungumza jambo mbele ya Mbunge wa jimbo hilo Patrobas Katambi
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi akiwakwenye kikso hicho
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM wilaya
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa baraza la jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Katibu wa CCM wilaya anayesimamia chama na Jumuia zake akizungumza kwenye kikao cha Baraza hilo.