Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao cha baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini
Suzy Luhende Shinyanga press blog
Wajumbe wa baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini wamempongeza katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya Doris Kibabi kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na kamati ya utekelezaji kwa kuanzisha miradi mbalimbali kwa muda mfupi yenye thamani ya Sh 9.3 milioni ukiwemo mradi wa ununuzi wa mashine mbili za kufyatulia tofali.
Pongezi hizo wamezitoa leo kwenye kikao cha baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini baada ya kuzungumzia miradi ya maendeleo iliyopo na iliyoanzishwa kwa muda mfupi ukiwemo mradi wa ufyatuaji matofali ambao unstarajiwa kuanza hivi ksribuni katika kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa wajumbe hao Jimotoli Jilala ambaye ni mjumbe wa kamati ya mipango uchumi na fedha katika jumuiya hiyo amesema anampongeza katibu pamoja na kamati yake kwa kuendelea kufanya kazi nzuri na kuanzisha miradi mikubwa kwa muda mfupi ambayo ilikuwa haipo.
"Tunakushukuru sana katibu wetu kwa kuendelea kutuheshimisha katika jumuiya yetu, kwani tulikuwa hatuna miradi, lakini sasa kuna miradi, hivyo jumuiya yetu itaondokana na kuomba omba itajitegemea, ni fahari sana kuwa na viongozi kama wewe katika wilaya yetu,"alimpongeza Jilala.
Tabu shabani mjumbe wa jumuiya hiyo wilaya amesema alichokifanya katibu Doris Kibabi kwa kushirikiana na kamati ya utekelezaji ni kikubwa sana ambacho kimefanyika kwa muda mfupi zamani walikuwa wanadharaulika hawasaminiki wazazi, lakini kwa sasa amerudisha heshima na kurudisha thamani ya wajumbe na wanachama, kutokana na hali hiyo wameuomba uongozi wa makao makuu wasimuondoe Shinyanga ili aendelee kufanya mazuri zaidi.
Sheka Ngusa katibu kata ya Kolandoto amesema baada ya kuanza kazi mkoa wa Shinyanga amehamasisha viongozi wote wakata kuanzisha miradi na kata nyingi zimeanzisha miradi ya ufugaji, zingine zimenunua viwanja kwa ajili ya kujenga mabanda ya biashara, wajumbe wengi walikuwa hawahudhulii kwenye vikao na sasa wanahudhulia kwa wingi
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko amesema pamoja na pongezi hizo walizozitoa wajumbe wanatakiwa kila kata matawi waendelee kuingiza wanachama wengi ili ifikapo mwaka 2025 waweze kuwa na wanachsma wa kutosha kwa ajili ya kupata ushindi wa kishindo .
"Niwaombe sana viongozi wangu kila mmoja afanye majukumu yake ili tuhakikishe kaya zote zinapata kadi za wazazi, acheni uvivu fanyeni kazi na kuhakikisha wanachama wote wanalipa ada kwa wakati ili waweze kuwa hai kwani wajibu wa mwanachama ni kulipa ada kwa hiari yako usisubiri kulazimishwa, sisi viongozi tuwe wa kwanza kulipa ada ili tuweze kuhamasisha na wanachama wetu walipe kwa wakati,"amesema Mlindoko.
Akisoma taarifa ya jumuiya hiyo Kibabi amesema Jumuiya hiyo ina mali zina zohamishika na visivyohamishika ambavyo ni viwanja 11 viwili vikiwa vya wilaya ambavyo wanavipata kutokana na ushirikiano wa viongozi wa wilaya na kata .
"Mwezi ujao tunatarajia kuanza ufyatuaji wa tofari kwa kutumia mashine zetu ya umeme na ya mkono kwani tayari umeme tumeshavuta ambao tumetumia jumla ya zaidi ya Sh 2 milioni ambao ni umeme wa viwandani, hivyo tunafanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wangu ndio maana mafanikio haya yanaonekana"amesema Kibabi .
Tutakapo anza ufyatuaji tofari wananchi wa Shinyanga watanufaika na tofari ambazo zitakuwa na kiwango kikubwa na jumuia itafaidika kujiongezea kipato na kupunguza kuombaomba tutakapokuwa na shughuli zetu, pia viongozi wangu wamenipongeza kutokana na mafanikio yanayoonekana tuliyoyafanya kwa muda mfupi,"
"Tangu nifike Shinyanga nimefanya uongozi shirikishi kwa ushirikiano na kwa uwazi hivyo ndiyo maana viongozi wangu wamenishukuru kutokana na weledi nilionao hivyo nitaendelea kuwashirikisha ili tuweze kufanya makubwa zaidi na kuijenga kwa upendo jumuiya yetu ,aliongeza Kibabi.
Katika kikao hicho alitambulisha viongozi wa kamati mbalimbali ambazo zimeteuliwa kwa ajili ya kusaidizana na kamati yautekelezaji ambazo ni kamati ya Uchumi, Afya, mazingira Elimu na malezi .
Katika baraza hilo mgeni rasmi alikuwa ni mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, ambaye aliwapongeza kwa kuwa na miradi hiyo ambayo itapunguza kuomba omba hivyo jumuiya itajitegemea hivyo kila kiongozi aweze kusimamia miradi hiyo, na kutafuta masoko na wanunuzi
Naye katibu elimu malezi na mazingira Salum Bandola amewataka viongozi wote na wanachama kupendana na kushirikiana katika kuijenga jumuiya na Chama na kuhakikisha kila mmoja anafanya kazi yake , makatibu walezi waendelee kuelimisha jamii kuachana na ukatili wa kila aina watoto waliofaulu wapelekwe wote shule na wanaostahili kuandikishwa waandikishwe.
Katibu wa wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi akizungumza na wajumbe wa baraza
Katibu wa wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi akizungumza na wajumbe wa baraza
Katibu wa wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi akizungumza na wajumbe wa baraza
mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao cha baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu akizungumza kwenye kikao cha baraza cha wazazi
Katibu elimu malezi na mazingira Salum Bandola ambapo amewataka wajumbe wote kupendana Jimotoli Jilala ambaye ni mjumbe wa kamati ya mipango uchumi na fedha katika jumuiya hiyo akizungumza ambapo aliahidi kushirikiana kikamilifu na viongozi wa jumuiya hiyo
Mary Makamba mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga
Mary Makamba mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo akiwa na viongozi wake
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu akimkabidhi cheti cha pongezi Katibu kata wa jumuiya ya wazazi Zuhura KondoKatibu elimu malezi na mazingira Salum Bandola skikabidhiwa cheti cha pongezi na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu akimkabidhi chet cha pongezi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Anold Makombe
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Ally Majeshi akikabidhiwa cheti cha pongezi na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji James Jumbe akikabidhiwa cheti na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu akisakata rumba na viongozi wa jumuiya ya wazazi
Wajumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao

Kazi ikiendelea Piter ambaye ni mjumbe wa baraza hilo
Mjumbe akiwa kwenye kikao hicho akifurahia jambo
Wajumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464