Mbunge wa jimbo la Msalala akiongelea kuhusu huduma ya maji.
Na Kareny
Masasy, Msalala
MBUNGE wa jimbo la Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Iddi Kassimu amesema yuko sambamba na Rais Samia Suluhu kumtua mama ndoo kichwani huku akimtaka meneja wa wakala wa maji safi na mazingira vijijini (Ruwasa) kumuandikia barua waziri wa maji ilia je kuzindua.
Mbunge Kassimu amesema hayo jana wakati wa ziara ya viongozi wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga walipotembelea mradi wa maji uliopo kwenye kijiji cha Busangi wakiongozwa na mbunge viti maalum Santiel Kirumba.
Mbunge Kassimu amesema wamekuwa wakishirikiana na mbunge wa viti maalum Santiel Kirumba kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi Msalala.
“Leo tupo kijiji cha Busangi mradi huu ulikuwa ukisuasua kukamilika ulianza tangu mwaka 2021 lakini sasa umesimamiwa vyema na umekamilika utaanza kufanya kazi niwatoe hofu maji mtapata na ushauri wa diwani nimeupokea”.
Mbunge Kassimu amesema meneja wa Ruwasa Julitte Payovela amekuwa akijitahidi katika utekelezaji wa miradi na siku ya uzinduzi wa mradi huu hakika atamzawadia ng’ombe amefanya kazi kubwa.
Mbunge Santiel amesema kwenye kata hii kweli wananchi wamepata shida ya maji,wengine kuugua kutokana na ukosefu wa maji safi na salama na wakati mwingine kuyatoa umbali mrefu wa zaidi ya kilomita tano lakini mradi mmeletewa na leo viongozi wamepita kuja kujirizisha kama fedha za maji zimefika.
“Rais Samia Suluhu Hassan anafahamu changamoto hii ndiyo maana ametutuma wabunge wa mkoa wa Shinyanga na viongozi wa chama kuja kutembelea na kuhakikisha fedha zimefika na ilani inatekelezwa”amesema Kirumba.
Diwani wa kata ya Mwalugulu ambaye ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga amesema wabunge Iddi Kassimu na Santiel Kirumba wamefanya kazi kubwa wameweza kusukuma gurudumu la maendeleo kwani kulikuwa na shida kubwa ya maji maeneo mengi na sasa hakuna tena.
Diwani wa kata ya Busangi Alexander Mihayo amesema mradi wa maji ukianza rasmi baadhi ya vitongoji vinaweza kukosa maji kulingana na jiografia ilivyo hivyo alishauri vichimbwe visima vifupi au virefu ili waweze kufikiwa na maji kwa haraka.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kahama Paschal Mnyeti amesema ujenzi wa mradi wa maji Nduku-Busangi –Nyamigege utakuwa na tanki lenye mita zaujazo 100 na vituo 16 vya kuchotea maji na vimekamilika kwa asilimia 97 na vitanufaisha wakazi 11,630Viongozi na wananchi wa kijiji cha Busangi wakishangili matumaini ya kupata huduma ya maji.Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akiwa na mwenyekiti wa UWT mkoa Grace SamweliMbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akiwa na mwenyekiti wa UWT mkoa Grace Samweli
Mbunge wa jimbo la Msalala Iddi Kassimu akiongea kuhusu upatikanaji wa maji kata ya Busangimaji yamekaribia kata ya Busangi kuzinduliwa hivi karibuni.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464