Taasisi isiyo ya Kiserikali ya World Sustainable initiatives kwa kushirikiana, MBRC Tanzania, HUDEFO, Mazingira Plus, taasisi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wamefanya usafi katika ufukwe wa bahari eneo la Geza Ulole ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru ambapo Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza katika maadhimisho haya kila Mkoa ufanye shughuli mbalimbali za kimaendeleo hii ikiwa ni moja wapo.
ETE pamoja na kushiriki kufanya usafi katika eneo hilo wanatumia Dijitali kuyasemea mazingira ambayo hayawezi kujisemea yenyewe, kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni kwa lengo la kufikisha ujumbe wa kukumbusha jamii kuendelea kutunza mazingira na kuyapenda ili yaendelee kuwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Picha na Fredy Njeje wa ETE insta @official.ete