MWENYEKITI WA UWT SHINYANGA MJINI AWATAKA VIONGOZI WA UWT KUSHIKAMANA NA KUKEMEA UKATILI

Mwenyekiti wa UWT CCM Wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha baraza wilaya ya Shinyanga mjini

Suzy Luhende, Shinyanga, press Blog

Mwenyekiti wa Umojawa wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewataka wajumbe wa baraza kushikamana na kuweza kuelimisha viongozi wa ngazi ya chini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaimalisha usalama kwenye mitaa yao katika kuijenga Jumuiya na Chama, ikiwa ni pamoja na kukemea ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Hayo ameyasema leo kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini ambapo amesema kila kiongozi ajue wajibu wake wa kazi huku akishirikiana na viongozi wenzake na kuelimishana ili kuhakikisha wanaijenga jumuiya na chama chake katika maeneo yao.

"Niwaombe sana viongozi wangu kila mmoja atambue kuwa yeye ni kiongozi amechaguliwa kwa ajili ya kuitumikia jumuiya yake tufanyeni kazi kwa kasi ya mama yetu mama Samia, ambaye anafanya kazi usiku na mchana, anafikilia kuifanyia maendeleo nchi yake, hivyo na sisi tufanye kazi kwenye kata zetu kwa bidii,"amesema Nhamanilo.

Pia Nhamanilo amewataka wajumbe wa baraza kwa sababu wao ni wanawake na ni walezi wawe walezi kwa watoto wote wanapoona wanawake wenzao au watoto wa jirani watoe taarifa ili wanaowafanyia ukatili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

"Wanawake wenzangu niwaombe tusimame sisi kama wanawake ili kulinda wanawake na watoto wetu wanaofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali ili kwa baadae tuweze kuwa na viongozi bora wanaojiamini, mtoto tukimuacha akifanyiwa ukatili baadae hawezi kuwa kiongozi mzuri kwa kuwa atakuwa na msongo wa mawazo, hivyo hata masomo yake hawezi kusoma vizuri,"amesema Nhamanilo.

Kwa upande wake katibu wa umoja wa wanawake UWT Shinyanga mjini Sharifa Mdee amewashauri wajumbe hao kuboresha taarifa zao kuanzia kwenye matawi, na waende wakaimalishe na kuhamasisha wanawake waweze kujiunga kwenye UWT na kuhakikisha wote wanalipa ada ili waweze kuendelea kuwa wanachama hai.

Kwa upande wake mjumbe wa baraza la UWT Taifa Christina Gule amewataka wajumbe hao kuungana, kushirikiana kuwa wamoja na kuheshimiana ikiwa ni pamoja na kuacha kunyanyasana wadumishe upendo ili kuijenga Jumuiya ya UWT na chama chake.

"Niwaombe wanawake wenzangu tupendane tusameheane pale tunapokwazana, kwani tukipendana tutafanya mambo makubwa kwa sababu sisi wote ni wa jumuiya moja na ni wanaCCM wote tukiungana tutafanya kazi zetu vizuri na kuwa na ushindo wa asilimia 100,"amesema Gule.

Naye Meya wa manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akizungumza kwenye baraza hilo amesisitiza upendo kwa wanawake na kuombana msamaha na kubebana ili waweze kukivusha chama cha mapinduzi kwa kupambana kwa pamoja na kuhakikisha CCM inavuka.
Mwenyekiti wa UWT CCM Wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha baraza wilaya ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akiwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban wakifuatilia taarifa zilizoandikwa kwenye makablasha
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Mdee akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Mdee akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya
Mjumbe wa baraza la UWT Taifa Christina Gule akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini

Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa Hamisa Maguru akizungumza kwenye kikao cha baraza
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa wa Shinyanga Mpaji Mwalimu akizungumza kwenye kikao cha Baraza la UWT wilaya
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Magdalena Dodoma akizungumza kwenye kikao cha baraza la Shinyanga Mjini
Naibu meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini wakifuatilia makablasha kwenye kikao cha baraza kwa umakini zaidi
Wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini akizungumza

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464