Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake UWT Shinyanga vijijini Mektrida Kenuka akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijini
Na Suzy Butondo, Shinyanga
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Mektrida Kenuka amewataka wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijini kusimamia kikamilifu majukumu ya Jumuiya ya wanawake na Chama ikiwa ni pamoja na kuhakuhakikisha wanatatua kero mbalimbalimbali zilizopo katika maeneo yao.
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo aliwataka kutekeleza majukumu yaokwa wakati na kutatua kero mbalimbali zilizopo katika maeneo yao.
"Leo tumefundishwa vitu vingi vya kufanya kwenye baraza hili niwwombe sasa tusiyaache hapa tukayafanyie kazi haya yote tuliyoelezwa na kukumbushwa kila mmoja akatimize wajibu wake kazi tuliomba sisi wenyewe kwa upendo, hivyo tukafanye kazi kwa upendo"amesema Kenuka
Kenuka aliwataka wajumbe wa baraza kujitambua na kufanya kazi zao za UWT kwa wakati huku wakiwaelekeza wajumbe wa matawi na kuelimishana pale ambapo haelewi ili kuujenga umoja wa wanawake na chama.
"Niwasihi viongozi wangu mnapofanya kazi zenu mnatakiwa kusaidizana elekezaneni mshirikiane na madiwani wetu wa viti maalumu, pamoja na wabunge wetu, ili kuhakikisha tunasimama imara katika umoja wetu na kuhakikisha mnafanya makubwa zaidi katika kata na wilaya,"aliongeza Kenuka.
Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Magdalena Dodoma aliwataka wale ambao hawajalipa ada walipe kwa wakati ili wawe hai, na waendelee kujisajili na kuhamasisha wanawake kujiunga na UWT na wale ambao hawajaanzisha miradi yoyote kwenye kata zao waanzishe ili kuondokana na kuombaomba.
" Niwashukuru sana makatibu kwa kazi mnazozifanya lakini niwaombe makatibu wote tutimize wajibu wetu kwenye majukumu yetu, kila mmoja ajue wajibu wake asisubiri kusukumwa kwani kila mmoja aliomba kazi hii kwa kujua kwamba anaweza kuitumikia na niwaombe mkahamasishe wanawake waweze kugombea nafasi za serikali za mitaa na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura pindi zoezi litakapoanza ,amesema Dodoma
Aidha mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT CCM Mkoani Shinyanga Grace Bizulu amewataka wanawake kuwalinda watoto wao wasifanyiwe ukatili, ikiwa ni pamoja na kuwajali waume zao ili kulinda ndoa zao.
Amesema baadhi ya wanaume wamekuwa wakilalamika kuwa hawapewi haki yao ya ndoa na wenza wao kwa sababu wako bize na shughuli zao, hivyo amewataka wanaofanya hivyo wabadilike wahakikishe wanawapenda na kuwajali wawape haki yao ya ndoa ili wasiendelee kulalamika.
"Na tunapowanyima tendo la ndoa waume zetu tunawasababisha wanaenda kwa michepuko hivyo tubadikike tuhakikishe tunalinda ndoa zetu ipasavyo,tukifanya hivyo tutapunguza kuwa na watoto wa mitaani,"amesema Bizulu
"Niwaombe wanawake wenzangu msijisahau mkawatelekeza waume zenu rudisheni upendo wa zamani, na walindeni watoto wenu ili wasifanyiwe ukatili kwani ukikaa bize na shughuli zako ukasahau kuzungumza na mtoto na kumuelekeza kwamba hiki ni kibaya atafanyiwa ukatili, lakini ukifanya kazi zako na kuwakumbuka watoto kuwafundisha hiki ni kizuri na hiki si kizuri atakuwa na maadili mema hatakubali kudanganywa kwa kuwa atakuwa na ukweli,"amesema Bizulu

"Pia sisi wanawake ni wawakilishi wa Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu, hivyo tunatakiwa tukaitangaze miradi mbalimbali ambayo anaifanya Rais wetu ili wananchi waweze kujua, kwani kuna baadhi ya wananchi hawajui anachokifanya na tumtangulize Mungu kila wakati ili tuwe na hofu ya Mungu, tukifanya hivyo tutafanya mambo makubwa na kulinda umoja wetu"amesema.
Naye mbunge viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava amewataka wajumbe wa baraza waweze kuunda kikundi cha SACOS, kwa kunza kujichangisha 5000 kwa mwezi, kwani kuna fursa benk inaweza ikawawekea fedha hata shilingi milioni 10 hadi 20 wakaanza kukopeshana.
"Mkikaa vizuri kila mwezi mnajiwekea 5000 mkatafuta mfadhili akawasaidia shilingi milioni 3 mtaanza kukopeshana hapa mliahidiwa shilingi milioni 10 na mbunge mmoja, lakini atawasaidiaje bila kuanzisha SACOS , hivyo niwaombe muunde kikundi cha SACOS mimi najitolea kuwa mlezi wenu, kinachotakiwa ni kuchagua mwenyekiti katibu na mtunza hazina,"amesema Mnzava.
"Na mimi niwasawishi muunde SACOS ya Shinyanga vijijini namimi najitolea kuwa mlezi namba moja ili ziweze kutusaodi pale tutakapokuwa na mahitaji mbali mbali"ameongeza Mnzava.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mektrida Kenuka akizungumza kwenye kikao cha baraza
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Magreth Dodoma akitoa maelekezo kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya.
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Magreth Dodoma akitoa maelekezo kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijini.
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Magreth Dodoma akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akizungumza kwenye kikaocha baraza hilo
Diwani viti maalumu wa wilaya ya Shinyanga vijijini Helena Daud akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT
Wajumbe wa kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijini wakiendelea na kikao hicho
Wajumbe wa kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijini wakiendelea na kikaohicho

Mbunge viti maalumu Christina Mnzava akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijni
Mbunge viti maalumu Christina Mnzava akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga vijijini
Mbunge viti maalumu Christina Mzava akikabidhi daftari la Taarifa ya wanachama wa Jumuiya ya wanawake wilaya ya Shinyanga vijijini kwa makatibu wa kata zote 26 za Shinyanga vijijini.