Na Kareny Masasy,Dodoma
RAIS wa muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema waandishi wa habari wameanza kuwa wabunifu kwenye klabu zao jambo ambalo litaweza kuondoa utegemezi waliokuwa nao nakufanya shughuli za kuisaidia jamii.
Hayo yamesemwa leo tarehe ,Desemba,2023 katika maonyesho ya shughuli zinazofanywa na vilabu vya waandishi wa habari 28 nchini sanjari na kuibua miradi ya kujinyanyua kiuchumi na kuazisha vikundi vya kukopa ambapo vinawasaidia kwenye kazi zao isitoshe baadhi ya vyombo vya habari haviwalipi.
Nsokolo amesema uandishi wa habari haujaachwa sababu ya kiuchumi na zimeshiriki masuala ya kusukuma guruduma la masuala la afya na kuweza kufanya kampeni na hatua nyingine mwandishi anaweza kuwa msaada kuikomboa jamii.
“UTPC imeweza kusaidia vilabu kulipia kodi za ofisi lakini tumeona zimeanza kuwa imara kwa kumiliki viwanja na mawazo haya vilabu ambavyo havina wayachukue ili baadaye kuja kuondokana na ufadhili”amesema Nsokolo..
Nsokolo amesema katika maonyesho hayo wameona vitabu mbalimbali vinavyotumiwa kama rejea kwa waandishi wanapoandika habari zao,sera na mwandishi anapoandika inaleta tija na kuona vilabu kusaidia mwandishi mmoja mmoja kuandika habari zenye mrengo anaouhitaji.
“Maandalizi ya maonyesho haya yamefanyika ndani ya mwezi mmoja lakini vilabu vimeitika kwa kuonyesha uwezo wao na namna wanavyo viripoti”amesema Nsokolo..
Mkurugenzi wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya amesema wote mashahidi klabu zinaweza kufanya kazi hivyo mwakani mambo makubwa yatakuwa bora zaidi jambo la msingi ni namna ya kupata maboresho ikiwa upo ubinifu na utajiri kwenye kila klabu ya waandishi.
“Hivyo tunawapongeza wafadhili wetu ambao ni SIDA na mwakani tutakuwa na maonyesho kwa kuwashirikisha watu wa kutoka nje na tasnia ya habari ili waje wajionee namna ya ushirikiano wetu”amesema Simbaya.
Mwakilishi kutoka shirika la Twaweza Jane Shusha amesema wamekuwa wakishirikiana na vyombo vya habari na kuimarisha sekta ya habari hivyo wameona mambo makubwa yakifanyika na vyombo vya habari vinaweza kujitegemea na kutatua migogoro.
“Katika maonyesho nimeona miradi mikubwa mmetekeleza na hivyo inawafanya kukuza taaluma yenu nimeona upo mwamko mzuri wa waandishi wa habari kutaka kujifunza na utayari wa kwenda mbali na mabadiliko yanayotokea kidijitali”Shusha.
Baadhi ya viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari nchini ambo ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru amesema Vilabu vimekuwa vikipaza sauti za wananchi na kuziandika kwenye vyombo vya habari ambapo serikali na wadau kuzitafutia ufumbuzi na kuzitatua.
Mwekahazina wa klabu ya waandishi wa habari kutoka visiwani Zanzibar Rahima Suleiman amesema maonyesho haya amejifunza namna ya klabu zingine zinazofaya kazi za mradi mbalimbali ambapo wengine wameanzisha vikundi vya vikoba na bodaboda.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi Fatuma Maumba amesema walichoona watakwenda kuboresha kwenye klabu yao kwani maonyesho haya yangeanzishwa zamani wangejifunza zaidi.