SERIKALI IMEELEZA KUTAMBUA HALI DUNI YA UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI

 Mkurugenzi wa  Idara ya Habari Maelezo na msemaji mkuu wa serikali . 

 Kareny  Masasy -Dodoma.

 SERIKALI  imeeleza  kutambua  changamoto  ya hali duni ya uchumi kwa vyombo vya habari na waandishi hapa nchini na imeanza kuchukua hatua ili kuhakisha kuna ustawi na ukuani wa maendeleo kwa Taifa na jamii na ameomba watendaji wa serikali kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari .

 Mkurugenzi wa  Idara ya Habari Maelezo na msemaji mkuu wa serikali   Mobhore  Matinyi   amesema hayo katika Mkutano  Mkuwa wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) alipokuwa mgeni rasmi.

Matinyi amesema  uchumi wa vyombo vya habari ulianza toka miaka ya 1995 na limekuwa kubwa zaidi kadri ya mabadiliko  ya teknolojia  na janga la UVIKO-19 lilipoingia duniani.

Matinyi  amesema   kumekuwepo na  uzito kwa baadhi watendaji wa serikali kutotoa ushirkiano kwa vyombo vya habari. 

 Matinyi amesema hali duni ya uchumi wa vyombo vya habari unaweza kuathiri sekta mbalimbali kwa kuwa hazitaweza kutangaza fursa za serikali kwa kuwa yapo maeneo ni ngumu waandishi kufika na kuiokosesha jamii haki ya kupata habari.

 "Dunia inakimba kwa teknolojia  na hakuna matangazo kwa vyombo vya habari kwa wingi,wateja wanatumia mitandao ya jamii kutangaza bidhaa na huduma zao na janga la UVIKO -19 ilibadili utamaduni wa watu kutumia mitandao zaidi kupata kwa ajili huduma na bidhaa" amesema Matinyi.

 "Kwa hali ya sasa ata uzalishaji  wa nakala za magazeti wa siku hauwezi kufikia nakala laki moja nchini kutokana mabadiliko"amesema Matinyi.

 Matinyi amesema serikali itakamilisha mchakato wake wa utafiti wa hali duni  kiuchumi kwa vyombo vya habari na kuweka mpango maalum kwa kuweza kutatu cha changamoto  hii" 

 Matinyi amesema baadhi ya wakurugenzi  serikalini wanachelewesha utoaji taarifa za msingi kwa vyombo vya habari zilizo na  tija kwa wananchi.

 Matinyi  amesema,serikali itaendelea kushirikia na vyombo vya habari kwa mafanikio yamekuwa na makubwa kwa nguvu ya vyombo vya habari.

"Sekta ya utaalii imefikia malengo zaidi baada  vyombo vya habari kutangaza filamu ya Royal Tour na kuleta idadi kubwa ya watalii katika hifadhi zetu" amesema Matinyi.


 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464