SHIRIKA LA FIKRA MPYA LIMEHITIMISHA JUKWA LA VIJANA ‘YOUTH CAFE’ CHUO CHA KIZUMBI

SHIRIKA LA FIKRA MPYA LIMEHITIMISHA JUKWA LA VIJANA ‘YOUTH CAFE’ CHUO CHA KIZUMBI

VIJANA 165 wenye umri kati ya miaka 12 hadi 25,wamefikiwa na Jukwaa la Vijana(YOUTH CAFE)kutoka Shirika lisilo la kiserikali la FIKRA MPYA,katika Manispaa ya Shinyanga na kuwapatia elimu ya afya ya uzazi,maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU),elimu ya kifedha na kujitambua.

Akizungumza leo wakati wa kuhitimisha jukwaa hilo,katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi-Taasisi ya Elimu ya Ushirika Kizumbi Tawi la Shinyanga,Mkurugenzi wa Shirika hilo Leah Josiah,amesema Jukwaa la Vijana(Youth Café)lilianza septemba 16-2023 na kumalizika leo Desemba 8,likiwa na lengo la kuwajenga vijana wa kike na wakiume walio ndani ya shule,nje ya shule pamoja na vyuoni kujikwamua kiuchumi na kubadilisha fikra zao.
Amesema kupitia jukwaa hilo,Shirika la Fikra mpya limewsaidia vijana kuelewa fursa zilizopo kwenye mazingira yao,kuwakutanisha na watu waliofanikiwa,kubaini changamoto zinazowakabili vijana na kuzitatua pamoja na kuleta usawa kwa ajili ya mabadiliko ya wote.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Bw.Tedson Ngwale akiongea wakati wa kufunga Jukwaa la Vijana amewasihi vijana na wanachuo katika chuo Kikuu cha Ushirika Moshi-Taasisi ya Elimu ya Ushirika Kizumbi Tawi la Shinyanga,kuwa waadilifu ambapo Meneja wa Jambo Media Nickson George akiwasihi kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya mambo chanya na kutafuta fursa.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dk. Paulin Paul amewasihi vijana wanaohitimu vyuo vikuu nchini,kutokutegemea ajira Serikalini na badala yake watumie elimu wanayopata kwenye vyuo vikuu kutambua na kutengeneza fursa zilizopo kwenye mazingira yao huku mratibu wa kudhitibiti Ukimwi Manispaa ya Shinyanga Salome Komba akisema maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoani Shinyanga kwa sasa ni asilimia 5.6,akiwataka vijana kujikinga na maambukizi hayo.

Shirika la Fikra Mpya lilipo mjini Shinyanga ambapo leo limehitimisha Programu yake ya Jukwaa la Vijana,yenye kauli mbiu isemayo”Jitafute,Jipate,Jitofautishe,likiahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuwainua vijana huku nao vijana wakishukuru kwa elimu nzuri waliyopatiwa na shirika hilo kuhusu afya ya uzazi,kutambua fursa za kiuchumi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye Jukwaa hilo.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa hilo.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa hilo.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa hilo.
Jukwaa la Vijana likiendelea katika Chuo Cha Kizumbi.

Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464