Mmoja wa wafanyakazi wa TRA akimuona mgonjwa wodini.
Na Kareny Masasy,Kahama
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kikodi Kahama, umekabidhi msaada wa Vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Jamii ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Shukran kwa Mlipa Kodi.
Akizungumza hayo leo tarehe 1/Desemba/2023 mara baada ya kukabidhi msaada huo Mwakilishi wa meneja kutoka mkoa wa Kikodi Kahama, Wisaka Kamwamu amesema kuwa msaada huu ni sehemu ya kutambua mchango unaotolewa na Jamii.
Kamwamu akikabidhi msaada huo amesema TRA itaendelea kufanya hivyo katika
Maeneo mengine kwa shukrani ambayo wameendelea kushirikiana na jamii.
Akipokea Msaada huo kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Dk Allan Masanja ameishukuru TRA kwa Msaada huo.
Ikiwa wametoa Magodoro ambayo ameeleza yatakwenda kusaidia maeneo muhimu kutokana na hospitali hiyo kuwa na idadi ya wagonjwa wengi kulazwa na wanaohudumiwa
Masanja amewataka wadau wengine kujitokeza kutoa msaada kwa ajili ya wenye uhitaji.
Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na Magodoro 30, Juice, Maji, Miswaki na vitu vidogo tofauti kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi tofauti tofauti.
Wafanyakazi wa TRA mkoa wa kikodi KahamaKama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464