UTPC YAFANIKISHA KUENDESHA KAMPENI MAALUM YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI KWA NJIA YA MTANDAO




 Afisa programu Maendeleo ya klabu na Utawala kutoka UTPC Hilda Kileo
 
Kareny Masasy,Dodoma 

MUUNGANO wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) wamefanikisha kuendesha kampeni maalum ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi wasichana na wanawake ambapo jumla ya maoni 1056 wameyakusanya yakizungumza  masuala ya ukatili.

Hayo yamesemwa leo tarehe 10,Desemba,2023 na Afisa programu Maendeleo ya Klabu na Utawala kutoka UTPC Hilda Kileo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu ambapo mgeni rasmi alikuwa Mobhare Matinyi.

Kileo amesema UTPC iliendesha kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa dhidi ya wanawake na wasichana kupitia mitandso ya jamii na vyombo vya habari na kuweza kubaini mikoa 5 iliyo ju kwa matukio ya vitendo vya ukatili

“Katika kamepni hii tumegundua mikoa ya katavi,Rukwa,Morogoro,Simiyu na Mara ndiyo imeongoza kuwa na taarifa nyingi za vitendo vya ukatili hasa kwa wanawake na wasichana.”amesema Kileo.

Kileo amesema UTPC ilishirikiana na viongozi mbalimbali na wadau baadhi katika kuendesha kampeni hii ikiwamo wabunge,wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kupitia mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti.

“Tunamini kupitia viongozi hawa jamii inajifunza kuhusu masuala ya ukatili kwa kutambua ushawishi walionao katija jamii”amesema Kileo.

Aidha,Wachangia mada walitoka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania kupitia jukwaa la kampeni hiyo walibainisha mambo kadhaa yanayochangia vitendo vya ukatili ikiwa ni ukosefu wa malezi bora,ukosefu wa saikolojia ya afya ya ubongo,mila na desturi na athari za kiuchumi.

Kileo amesema wachangiaji hao walibainisha mbinu zinazoweza kusaidia kupambana na ukatili ikiwa ni vyombo vya habari vitoe elimu,msaada wa kisheria kwa wanawake,uanzishaji wa vikundi vya kupambana na ukatili na jamii ipatiwe elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia.

“Kampeni hiyo ilipata hoja ya mtazamo wa baadhi ya wanaume kusema elimu ya ukatili imechukuliwa kama fimbo kwa baadhi ya wanawake na kulega katika wajibu w kutimiza majukumu ya ndoa na familia”amesema Kileo.

Kileo amesema UTPC imefanikiwa kuhitimisha kampeni hiyo kutokana na ushiriki mzuri na kutoa msukumo wa nguvu ya kuendelea na mapambano ili kuwa na jamii salama isiyoweza kuathiriwa na ukatili kwa mtu yeyote kwa ngazi ya familia,jamii na Taifa.   

Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo amesema  leo  inatimia miaka 75 ya kimataifa ya kupinga vitendo vya ukatili kwa kukiuka haki za binadamu  na sehemu ya UTPC imeshiriki kwenye kampeni  ya siku 16 za kupinga ukatili kwa nchi hii.


Wajumbe wa mkutano mkuu wa UTPC wakiwa kwenye mkutano

Mgeni rasmi kwenye  mkutano mkuu wa UTPC  Msemaji wa serikali na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Mobhare Matinyi.





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464