UTPC YATOA SALAMU ZA POLE KWA RAIS JANGA LA HANANG, MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AZIPOKEA


Mkurugenzi wa idara habari maelezo na msemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi.

 Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo.

Na Kareny Masasy,Dodoma

MKURUGENZI wa idara ya habari maelezo na msemaji mkuu wa Serikali  Mobhare   Matinyi  amesema  wizara 13 za Serikali  zimeshiriki katika kufanikisha kazi ya kurudisha  hali  na uokoaji wa  waathirika  kutoka Hanang mkoani Manyara.

 Ambapo amesema moja ya wizara iliyotumika ni wizara ya  ardhi,nyumba na makazi ambapo wametumia sensa ya watu na makazi iliyofanyiwa Agosti Mwaka 2022  kutambua makazi  kulingana na hali ilivyotokea  nyumba 100 zimebainika kusambaa kabisa.

 Matinyi amesema  hayo leo tarehe 10/Desemba.2023 kwenye mkutano mkuu wa muungano wa klabu za waandishi wa habari  nchini (UTPC) uliokutanisha klabu 28  ikiwa 26 kutoka Tanzania bara na mbili Tanzania visiwani alipokuwa mgeni rasmi  kwenye mkutano huo huku akipokea pole iliyotolewa  na Rais wa UTPC kuhusisha na janga lililotokea  eneo la Hanang  mkoani Manyara ambalo limeleta historia .

 Matinyi amesema  kazi ngumu imefanyika Hanang kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuleta misaada  ikiwa kulikuwa na majeruhi   139 hospitalini  lakini mpaka Sasa  kumebaki majeruhi 30.

 "Tope hilo  lilikuwa  likikimbia kilomita 6.1 lilikuwa likipitia nyumba moja na kuikumba nyingine  chanzo kimechunguzwa na kubainika kuwa  mchanga laini uliokuwa umejibumba na kuunda mlima ulikuwa unaloaana taratibu  na mvua iliyokuwa imenyesha sio kubwa" ame
sema Matinyi.

 Matinyi amesema   mpaka sasa   Kuna ripoti ya  vifo 87  na waliobahatika kupona wanasimulia hadithi  za kusikitisha na namna walivyo okolewa.

 Matinyi  amesema  Serikali kwa sasa imerudi  kwa mpango mkakati wa   kutarajia kuwapatia vifaa vya ujenzi  na kazi iliyofanyiwa niya utu na uzalendo mkubwa.

 Matinyi amesema  kila kitu kikitokea kina fundisho lake ambapo watu  wamepigwa marufuku  kuweka makazi  bali wameruhusiwa kuwa umbali wa kilomita 30 ili  wasipate madhara tena kama yalivyotokea.

 Rais  wa  muungano wa klabu za waandishi wa habari  nchini (UTPC) Deogratius Nsokolo alitoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan kufuatia majeruhi na vifo vilivyowakuta watu wanaoishi Hanang  mkoani Manyara.




 Mkurugenzi wa UTPC  Kenneth Simbaya akiongea kwenye mkutano mkuu

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464