UTPC YATOA TUZO ZA UADILIFU KWA WAANDISHI WA HABARI KWA MARA YA KWANZA


Waandishi wa habari sita pamoja na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa.
Washindi sita wa tuzo za uandilifu zilizotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2023 na UTPC
Kareny Masasy,Dodoma
 
WAANDISHI wa habari sita kutoka mikao tofauti wamepewa tuzo za uadilifu zilizoanza kutolewa rasmi mwaka 2023 na muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC).
Mwenyekiti wa tuzo hizo Chiku Lweno amesema hayo tarehe 10,Decemba,2023 kabla ya kutoa tuzo hizo kwa washindi ambapo ameeleza habari zilianza kupitiwa tarehe 5,Desemba kwa kuangalia uadilifu ,kanuni na maadili nakutoa habari za kweli kwa kina.

Lweno ametaja washindi hao sita ambao wamepata fedha taslimu na cheti ambao ni Rehema Evans kutoka mkoa wa Simiyu aliyeshika nafasi ya tatu upande wa wanawake nakujinyakulia sh Laki tano (500,0000, Mshindi wa pili Jackline Kawanda kutoka mkoani Dodoma aliyejinyankulia sh Milioni moja (1000,000) na mshindi wa kwanza ni Shukrani Kawogo kutoka mkoani Njombe aliyepata sh Milioni 1.5

Lweno aliwataja washindi upande wa wanaume ambapo mshindi wa tatu ni Marco Maduhu kutoka mkoani Shinyanga aliyepata sh 500,000,Mshindi wa pili ni Abdalah Bakari kutoka mkoani Mtwara aliyepata sh Milioni moja (1000,000) na mshindi wa kwanza Zacharia Nyamoga kutoka mkoani Iringa aliyepata sh Milioni 1.5

“Washindi wote hongereni kwa mchango wenu tunataka matokeo chanya kwani jumla ya habari 52 zilitumwa na kila moja ilipitiwa kwa kina na kujadiliwa na tumefanikiwa kutambua washindi na usiku huu tunawatangaza”.amesema Lweno.

Mkurugenzi wa UTPC Keneth Simbaya amesema mwaka 2023 hakukuwa na mshindi wa tuzo ya Mwangosi ambayo ilikuwa ikitolewa na UTPC na sasa wataleta utaratibu mwingine wa utolewaji wa tuzo kwa kazi za waandishi.

“Habari 52 zimeletwa na kupokelewa na majaji watatu kwa kutathimini na kuona uwajibikaji wa vigezo vilivyo wekwa na habari hizo zimekidhi na kupata kuteuliwa na zile ambazo hazijachaguliwa waandishi wake watapewa elimu zaidi namna ya kuziboresha”Simbaya.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na msemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi ambaye amekuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hizo amesema jambo la kupewa tuzo kwa kushinda ni kitu kizuri wapo waandishi wengi wanaoshinda na ambao hawashindi lakini wanajifunza kwa wengine.

Matinyi amesema zipo habari ambazo zimeweza kufanyiwa uchunguzi kwa muda mrefu na kubaini ukweli na serikali kuchukua hatua ni moja ya jukumu la mwandishi kufanya hivyo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464