Moja ya banda la klabu ya waandishi wa habari yakikaguliwa na wajumbe wa bodi ya UTPC.
Na Kareny Masasy,Dodoma
VIONGOZI wa Klabu za waandishi wa habari nchini wameeleza kubadilika kuendana na kasi ya kidijitali kutokana na maonyesho ya mabanda kwa mara ya kwanza kufanyika nakuonyesha namna ya ufanyaji miradi na shughuli kwenye maeneo yao kwa lengo la kuwakomboa waandishi.
Wakiongea kwa nyakati tofauti jana tarehe 9,Desemba,2023 wakati wa maonyesho viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoani Shinyanga Greyson Kakuru amesema maonyesho hayo yamewapa chachu kwenda kuboresha zaidi kwani wamekuwa wakipaza sauti changamoto za kwenye jamii kwa kushirikiana na wadau na serikali.
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoani Ruvuma Andrew Chatwanga amesema klabu zinasimamia vizuri majukumu ya waandishi wao na kujitahidi kuwanyanyua .
Akitolea mfano kwenye klabu yake amesema wameanzisha kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti ambacho kikianza kuzalisha waandishi watanufaika kwa kujinyanyua kiuchumi.
Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari Singida Domiciana Mwalusito amesema maonyesho hayo amejifunza kutoka kwenye mikoa mingine nini wamefanya ili nao waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya utekelezaji na kujinyanyua kiuchumi
“Tunaweza kuanzisha miradi na kuajiri watu wengine bila kutegemea UTPC kwani klabu tayari ni taasisi hivyo viongozi wakiweka nia tunaweza”amesema Mwalusito.
Mwekahazina wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoani Kagera Alodia Dominick amesema katika maonyesho haya amejifunza kwani kuna miradi mingi yakufanya.
“Sisi tunaendelea kubuni miradi tofauti tofauti na tumeshawishika kurudisha gazeti letu la zamani lililokuwa likiitwa malengo yetu na waandishi wa habari watapata fursa kulitumia”amesema Dominick.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoani Mwanza Edwin Soko anasema klabu zinafanya za kijamii na zinaendelea kupaza sauti nakuonyesha kesho yake itakuwaje,utayari wa kujifunza kutoka kwenye klabu zingine na kuwa na moyo wa kubadilika kwenda na dhana ya kutoka kwenye ubora na kuwa bora zaidi.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoa wa Rukwa Nswima Ernest amesema kwa mara ya kwanza waandishi wa habari wamekutana kwenye maonyesho kwa namna ya kujifunza kuna masuala ya kijamii na kiuchumi.
“Zipo klabu ambazo zimejipanga vizuri zimeonyesha malengo yake na tumejifunza hakuna mtu yoyote wa kukupa raha,raha unajipa mwenyewe.”amesema Ernest.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoa wa Geita Renatus Masuguliko amesema maonyesho haya yameibua hali ya kuleta ushindani na kujipima uwezo wake na mikakati waliyonayo ni kufikia malengo kwa kuchochea na kuibua miradi.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari kutoka mkoani Lindi Fatuma Maumba amesema amejifunza kutoka kwenye klabu zingine na wakitoka hapa wanakwenda kuboresha vya zamani na kuanzisha vitu vipya.
Mwekahazina
kutoka klabu ya waandishi wa habari Zanzibar amesema Rahima Suleiman
amesema maonyesho haya amejifunza kutoka kwenye klabu zingine zinavyfanya kazi zipo zilizoanzisha vikoba na
miradi ya pikipiki kwa kuona klabu zinaweza kuwasaidia wanachama kujikwamua
kiuchumi
Makamu mwenyekiti wa UTPC Pendo Mwakyembe akiweka saini kwenye moja ya banda la klabu ya waandishi wa habari kwenye maonyesho ya mabada na shughuli wanazofanya
Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo akiwa kwenye mabanda ya maonyesho yaliyoshirikisha klabu za waandishi wa habari mikoa yote 28
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464