WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI YA DHAHABU WAFUNGUA KESI YA MADAI DHIDI YA RAIS WA WACHIMBAJI

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Busega namba 2 Jumanne Guguye akizungumza baada ya kutoka mahakamani

Suzy Luhende Shinyanga press blog

Shinyanga. Wachimbaji wadogo wapatao 18 kutoka wilayani Busega Mkoani Simiyu wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wakimshtaki Rais wa Chama cha Wachimabaji wadogo wa Madini nchini FEMATA John Binna kwa tuhuma za kuleta Mwekezaji na kuharibu mali zao pasipo kuwalipa fidia, ambapo shauri hilo limeahirishwa hadi march 4 mwaka huu.

Shauri hilo namba 24 la mwaka 2023 limefunguliwa katika mahakama hiyo ambapo wachimbaji hao wanadai fidia ya mali zao zilizoharibika kwa kufukiwa ndani ya mgodi huo wakati wa zoezi la kuwaondoa kwa nguvu katika mgodi wa Busega Imaramate Namba 2.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Busega namba 2 Jumanne Guguye amesema vifaa vyao vilifukiwa bila kusikilizwa ambapo hawakuweza kuondoa kitu chochote katika eneo hilo ikiwemo vifaa na mitambo waliyokuwa wakitumia katika shughuli za uchimbaji vyenye jumla ya Sh 3.5 bilioni.

"Hawa watu ambao ni Raia wa kigeni waliowekwa kwenye maeneo yetu tuliyokuwa tukichimba wanafanya kazi kinyamera kwanza wanaibia serikali wanatumia leseni ya john wambura bina kwa sababu yeye ni m/kiti wa wachimbaji wadogowadogo tunaiomba serikali ilitazame kwa umakini suala hili"amesema Guguye.

"Nimepata vitisho vingi sana kutoka kwa Binna naiomba serikali itusaidie iliingilie suala hili ili tuweze kupata haki zetu, kwani tulitumia fedha nyingi zaidi ya bilioni tatu ambazo zimefukiwa ndani ya mashimo hayo"amesema Guguye.

Mmoja wa wachimbaji hao Joseph Samson Marwa amesema yeye alianza kuchimba katika eneo hilo toka mwaka mwaka 2020, lakini Jonh Binna alikuwa kiongozi wao ambaye alikuwa akiwasaidia na kuahidi kuwatafutia vifaa vya kukopa,lakini wanadai hivi karibuni mwaka 2021 amebadilika na kuanza kuwafukuza katika eneo hilo huku akifukia vifaa vyao bila kuwashirikisha.

"Sisi kama wachimbaji tunadai gharama zetu, lakini Binna alilipwa fedha ili atulipe, lakini mpaka leo hajatulipa chochote nayeye ndiye alikuwa mtetezi wetu lakini ametubadilikia na kuanza kutunyanyasa sisi, tunamuomba Rais Samia Suluhu atusaidie tuweze kupata haki zetu,"amesema Marwa.

Wakili wa wachimbaji wadogo Protas Katozake amesema shauri hili limefunguliwa Msoma kwa mara ya kwanza lakini ikaonekana mahakama hiyo haistahili kesi hiyo, ndiyo ikahamishiwa katika mahakama ya kanda ya Shinyanya ambayo inasimamiwa na Jaji Seif Kulita.

"Hapa Shinyanga tunalo shauri la wateja wetu wapatao 18 dhidi ya mdaiwa John Binna shauri namba 24/ la mwaka 2023 shauri hili lilikuwa linatajwa leo kwa mara ya kwanza lakini limeahirishwa kutokana na jaji kutokuwepo, hivyo lImeahirishwa hadi tarehe 4/3/2024 wadai wangu wanadai fidia zilizofukiwa katika mgodi mdogo wa Busega namba 2 ." chini ya uongozi wa mdaiwa Amesema Katozake.

"Hata hivyo mdaiwa hajafika mahakamani ila wakili wake alipokea wito, lakini pia shughuli zinaendelea kwenye mgodi huku vifaa vya wateja wangu vikiwa vimefukiwa katika eneo hilo lakini tuliomba shughuli za uchimbaji zisitishwe kwa sababu kuna vifaa vya wateja wangu katika eneo hilo lakini mpaka sasa tunaona uchimbaji unaendelea"ameongeza Bina



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464