RC MNDEME AMEFANYA ZIARA KUKAGUA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI KURIPOTI SHULE
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amefanya ziara ya kukagua mahudhurio ya wanafunzi ambao wamechanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, pamoja na uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza katika shule mbalimbali mkoani humo.
Ziara hiyo imefanyika leo Januari 8,2024 ikiwa ni siku ya kwanza ya kufunguliwa shule kwa kuanza masomo 2024, na kusikitishwa na Mmoja wa wazazi kutaka kukatisha ndoto za mtoto wake kwa kumuoza kwa mahari ya Ng’ombe 15 katika Kijiji cha Iyugi wilayani Shinyanga.
Mndeme akizungumza kwenye ziara hiyo, amewata wazazi na wale kuhakikisha watoto wao ambao wamechanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wote waripoti shule na hakuna hata mmoja kukosa, na wale ambao wamefikisha umri wa kuanza masomo ya awali na darasa la kwanza wawapeleke shule ili wapate haki yao ya elimu na kutimiza ndoto zao.
Amesema Rais Samia amekuwa akitafuta pesa ili watoto wasome bure, pamoja na kuimarisha miundombinu ya elimu na kuwataka wazazi wasimwangushe Rais, bali wapeleke watoto wao kwa wingi kupata elimu wakiwamo na wenye ulemavu pamoja na kuacha tabia ya kuozesha watoto ndoa za utotoni kwa tamaa ya mifugo na kuzima ndoto zao.
“Nawaomba wazazi pelekeni watoto wenu shule ili wapate elimu wakiwamo na wenye ulemavu msiwafiche ndani miundombinu ya shule ni rafiki kwao na elimu inatolewa bure,”amesema Mndeme.
“Nakemea pia tabia ya kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni, na mzazi ambaye alitaka kumuozesha mtoto wake wa Kidato cha kwanza kwa Mahari ya Ng’ombe 15 katika Kijiji cha Iyugi Kata ya Lyamidati, tunamsaka sababu amekimbia na akikamatwa tutamchukulia hatua kali za kisheria ili liwefundisho kwa wazazi wengine,”ameongeza Mndeme.
Aidha, amewataka Walimu kuendelea kufundisha kwa bidii ili wanafunzi wapate kuelewa masomo na kufanya vizuri kitaaluma, huku akiwasihi pia wanafunzi wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, ametaja idadi ya wanafunzi kimkoa ambao mpaka sasa wamesharipoti shule kwa siku ya kwanza, kwamba darasa la wali kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi (2022)maoteo ni kuandikisha watoto 75,079 lakini wamesha andikisha 47,182, darasa la kwanza watoto 69,792 na wameandikisha watoto 44,332, Kidato cha kwanza wanafunzi 38,963 lakini mpka sasa bado hawana takwimu wameripoti wanafunzi wangapi.
Aidha, shule ambazo ametembelea Mkuu wa Mkoa ni Shule ya Msingi Mwenye ambapo kwa siku ya kwanza wanafunzi wa Awali wameandikisha watoto 80 kati ya 156, darasa la kwanza wanafunzi 217 kati ya 230.
Shule ya Sekondari Ngokolo mpaka sasa wamesharipoti wanafunzi 79 kati ya 347, shule ya Sekondari ya wasichana wanafunzi walichaguliwa kujiunga ni 143 wamesharipoti 10.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa amembeba mtoto ambaye anasoma darasa la awali shule ya Msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa Madaftari na Kalamu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya Msingi Mwenge.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa Madaftari na Kalamu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya Msingi Mwenge.
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiwa darasani shule ya Msingi Mwenge.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa Madaftari na Kalamu kwa wanafunzi shule ya Sekondari Ngokolo.
Wanafunzi shule ya Sekondari Ngokolo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga.
Wanafunzi shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwa ziara ya kukagua mahudhurio ya wanafunzi kuripoti shule.