KATAMBI AMKABIDHI MAKONDA SH.MILIONI 2/-FEDHA KWA AJILI YA RAIS SAMIA KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS TENA UCHAGUZI MKUU 2025
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amemkabidhi fedha Sh,milioni 2 Katibu wa NEC,Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo hilo,fedha kwa ajili ya Rais Samia kuchukua Fomu kugombea Urais tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, amekabidhi fedha hizo leo Januari 28, 2024 kwenye Mkutano wa Makonda wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali na Chama.
Katambi akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo kwa niaba ya wananchi, amesema Rais Samia ameleta maendeleo Makubwa katika Jimbo la Shinyanga, na kutatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa sugu, hivyo wameona ni vyema kumpatia fedha hizo ili achukue fomu ya kugombea Urais tena na kuendelea kuwatumikia wananchi.
“Rais Samia amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Shinyanga ya sasa siyo kama ya zamani, ukiangalia hata miundombinu ya barabara imeboreshwa sana, Madaraja yamejenga ambayo yalikuwa kero kubwa kwa wananchi na sasa kero hiyo haipo tena,”amesema Katambi.
Ameongeza” Pia katika Sekta ya Afya amefanya maendeleo makubwa sana, Sekta ya Maji, Elimu,Umeme, Ujenzi wa Machinjio, Uwanja wa Ndege pale Ibadakuli, Ujenzi wa vyuo Vikuu, na sasa katoa tena fedha ambapo tunajenga Stendi Kubwa ya Mabasi na Soko la kisasa, nani kama Rais Samia…. hakuna,”.
Katibu wa Itikadi,Unezi na Mafunzo Paul Makonda, amewapongeza wananchi wa Shinyanga kwa kumpatia fedha Rais Samia kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais tena katika uchaguzi wa 2025 kutokana na kuwaletea maendeleo makubwa, na kuahidi kwamba fedha hizo zitafika na atamleta Rais Samia Shinyanga.
Aidha, Makonda katika Mkutano huo amezindua Rasmi Maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, yenye Kauli Mbiu isemayo Shiriki uchaguzi kwa uadilifu kazi iendelee.
Katika hatua nyingine amewataka Watumishi wa Serikali na Chama kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi, na kutatua changamoto zao mbalimbali ambazo zinawakabili.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (kulia) akimkabidhi Sh.milioni 2 Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Paul Makonda kwa ajili ya Rais Samia kuchukua fomu ya kugombea Urais tena katika uchanguzi Mkuu wa 2025.
Meza Kuu wakiwa kwenye Mkutano wa Makonda.
Mkutano wa Makonda ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Makonda.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464