SENET SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 60 YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA,KUCHANGIA DAMU KITUO CHA AFYA KAMBARAGE
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SENET ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Shinyanga kupitia Umoja wa vijana UVCCM, wameadhimisha miaka 60 ya mapinduzi matukufu ya Nzanzibar, kwa kufanya usafi wa mazingira na kuchangia damu katika kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Januari 12, 2024 ambayo yaliambatana na matembezi ya amani, pamoja na kufanyika Kongamano la vijana katika Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM).
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, amesema wameamua kuyaenzi kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa damu katika kituo hicho cha Afya Kambarage ili kuungana na wanzanzibar.
“Wazanzibar ni ndugu zetu hivyo sisi kama Senet Mkoa wa Shinyanga, tumeamua kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kufanya usafi wa mazingira na kutoa damu katika kituo cha Afya Kambarage,”amesema Sultan.
“Senet Mkoa wa Shinyanga tupo pamoja na viongozi wetu wa CCM pamoja na Rais DK Samia na Dk, Mwinyi huko Zanzibar na tunatambua kazi kubwa ambazo wanazifanya katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo,”ameongeza Sultan.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi, amewapongeza Senet ya Mkoa wa Shinyanga, kwa kufanya jambo hilo kubwa kwa kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar, kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa damu jambo ambalo ni jema na kuimarisha undugu na kuyaenzi mapinduzi.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Samweli Jackson, akizungumza kwa niaba ya Mbunge Katambi, amewataka vijana hao kutoka vyuoni wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao, ambapo Serikali chini ya Rais Samia itaendelea kuboresha mazingira rafiki ya wanafunzi kusoma.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kambarage Dk. Ernest Magula, amewapongeza vijana hao kutoka Senet kwa jambo hilo kubwa ambalo wamelifanya hospitalini hapo, na kutaja takwimu za damu ambazo zimechangiwa na vijana hao kuwa ni unit 25 na zitasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa damu salama.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mkoani Shinyanga yaliyoadhimishwa na Senet.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mkoani Shinyanga.
Katibu wa Senet Mkoa wa Shinyanga Masunga Mazoya akizungumza.
Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kambarage Dk.Ernest Magula akizungumza.
Mwenyekiti wa Chipukizi Mkoa wa Shinyanga Maimuna Said akizungumza.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akizungumza.
Zoezi la Usafi wa Mazingira Kituo cha Afya Kambarage likiendelea.

Zoezi la kuchangia damu Kituo cha Afya Kambarage likiendelea.

Wana Senet kutoka vyuo mbalimbali Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano, mara baada ya kumaliza kufanya Usafi wa Mazingira na kuchangia damu Kituo cha Afya Kambarage.
Kongamano la vijana kutoka Senet likiendelea.
Kongamano la vijana kutoka Senet likiendelea.
Matembezi ya Amani yakiendelea katika kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutoka Ofisi ya CCM Mkoa wa Shinyanga hadi Kituo cha Afya Kambarage.

Picha ya Pamoja ikipigwa.