TCRS WAMEENDESHA MAFUNZO KWA WAKULIMA KISHAPU KUONGEZA THAMANI KWENYE ZAO LA NYANYA NA KUTENGENEZA TOMATO "SAUCE"
Shirika la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) kwa ufadhili wa kifedha kutoka shirika la Norwegian Church Aid (NCA); limeendesha mafunzo yakuongeza thamani kwenye mazao hasa Nyanya, kwa wakulima pamoja na wadau wengine wa kilimo kutoka kata za Sekebugolo na Mondo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano kijiji cha Mwigumbi Wilaya ya Kishapu na kwamba yameandaliwa na shirika la TCRS huku wawezeshaji wakitoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga.
Wakulima 20 walioshiriki mafunzo hayo wamepewa vyeti wakiwemo wafanyabiashara wa zao la Nyanya kutoka kwenye vijiji vinne ambavyo ni Mipa, Dulisi, Weshiteleja pamoja na kijiji cha Sekeididi na kwamba wamepewa mafunzo mbalimbali ikiwemo usindikaji wa zao la nyanya ili kupata Tomato Sauce and Tomato Paste.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Afisa uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban amewasisitiza washiriki baada ya kupata elimu hiyo, kujiendeleza zaidi na ujuzi huo ili waweze kunufaika wao na jamii kwa ujumla.
“Baada ya mafunzo haya na leo hii tumetunukiwa vyeti yasiishie hapa hapa ni lazima tuhakikishe kwamba ujuzi huu tulioupata ukawe na manufaa kwetu na watu wengine wanaotuzunguka, hapa umepata ujuzi lakini ili uweze kuwa na manufaa, ujuzi huu ni wewe kuendelea kufanyia mazoezi hata kabla hujaanza kuanzisha hicho kiwanda kidogo cha usindikaji anza kusindika kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani kwanza halafu badaye utakavyokuwa unafanya mara kwa mara utakuwa unagundua na vitu vingine ambavyo hukujifunza awali”.amesema Taban.
Kwa upande wake afisa uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka SIDO Bwana Abel Bebwa amewasihi washiriki hao kujiamini zaidi kwenye utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika Maisha ya kila siku.
Naye afisa Kilimo kutoka shirika la TCRS Wilaya ya Shinyanga Bwana Laurent Stanslaus amezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo hasa kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao la Nyanya.
“Mafunzo haya yanalenga hasa kuweza kupunguza matatizo ambayo yanatokana na uharibifu wa chakula kwa sababu kuna muda wakulima wanavuna mazao mengi hasa mazao yanayowahi kuharibika mfano zao la Nyanya akivuna halafu unakuta soko ni changamoto kwahiyo tumeona kwamba tuwape mafunzo haya ili mkulima aweze kuwa na uwezo wa kufaidika na mazao anayoyapata”.amesema Stanslaus
Washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru TCRS, NCA pamoja na shirika la SIDO kwa kuwapa elimu hiyo ambayo wamesema itawasaidia kuinuka kiuchumi hasa katika Biashara pamoja na shughuli zingine za kwenye familia zao ikiwemo kusomesha watoto.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Afisa uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa katika maandalizi ya kuanza zoezi la usindikaji wa Sosi ya Nyanya.
Washiriki wakiwa katika maandalizi ya kuanza zoezi la usindikaji wa Sosi ya Nyanya.
Washiriki wakiandaa mahitaji muhimu ikiwemo vitunguu maji, Chumvi, Sukari, Pilipili manga kwa ajili ya usindikaji wa sosi ya Nyanya.
Maandalizi yakiendelea.
Mafunzo yakianza jinsi ya kutengeneza Sosi.
Mafunzo yakiendelea.
Muonekano wa Sosi.
Afisa Uendeshaji Biashara Mwandamizi kutoka SIDO Abeli Bebwa (kulia) akitoa vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo hayo.
Zoezi la utoaji vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo likiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Wahitimu wa Mafunzo hayo wakipiga picha ya pamoja na bidhaa zao ambazo wamezitengeneza za Sosi kupitia Zao la Nyanya.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464