MADIWANI SHINYANGA WAPITISHA MAPENDEKEZO MPANGO WA BAJETI MWAKA WA FEDHA 2024/2025 SH.BILIONI 40.3/-
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, limepitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha (2024/2025) kiasi cha fedha Sh.bilioni 40.3.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Mapendekezo ya Bajeti hiyo yamepitIshwa leo Januari 25, 2024 kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani, lililoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Michael Makotwe, akiwasilisha Mapendekezo ya mpango huo wa bajeti wa mwaka wa fedha (2024/2025), amesema wanatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha fedha Sh.bilioni 40.3 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
Ametaja vyanzo hivyo vya mapato, kwamba mapato ya ndani Makisio ni kukusanya Sh.bilioni 6, Ruzuku na matumizi mengine Sh.bilioni 1.3, Ruzuku ya Mishahara Sh.bilioni 23.3, Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali Kuu Sh. Bilioni 5.3 na Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo Wahisani Sh.bilioni 4.3.
Aidha, Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, mara baada ya madiwani kujadili mapendekezo ya bajeti hiyo na kuiridhia, alitamka Rasmi kwamba Baraza hilo la Madiwani limeipitisha Bajeti hiyo.
Akizungumza kabla ya kuhitimisha kikao hicho cha Baraza, amewataka Madiwani pamoja na watendaji waisimamie vyema bajeti hiyo, pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya, ili mipango ambayo imepangwa iweze kutekelezeka na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
“Bajeti hii inagusa maisha ya Wana-Shinyanga naomba tufanyeni kazi kwa uzalendo na tuwe wasimamizi wazuri, wananchi wanataka kuona matokeo katika utekelezaji wa Miradi,”Amesema Masumbuko.
Katibu Tawala sehemu ya Ufuatiliaji wa Menejimenti na ukaguzi Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana, amewataka Madiwani pamoja na Watendaji kwamba wasimamie,kudhibiti na kufanya ukaguzi wa mapato, na wale wanaokusanya mapato fedha wawe wanaziwasilisha Benki kwa mujibu wa muongozo na kanuni.
Nao baadhi ya Madiwani wakijadili Mapendekezo ya Bajeti hiyo, waliomba kwamba itakapoanza kutumika na mifumo kufunguka, watoe kipaumbele kwanza kwenye ufunguzi wa miundombinu ya barabara.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Kassimu Thadeo, amesema maoni yote ambayo yamejadiliwa kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani watayazingatia na kuyafanyia kazi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Kassimu Thadeo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Katibu Tawala sehemu ya Ufuatiliaji wa Menejimenti na ukaguzi Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Michael Makotwe, akiwasilisha Mapendekezo ya mpango huo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza la kujadili na kupitisha mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya akichangia mada kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Diwani wa Vitimaluum Shela Mshandete akichangia Mada kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Wataalamu wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464