RC MNDEME AZUNGUMZA NA WAZEE, MACHIFU NA VIONGOZI WA DINI KUCHOTA NASAHA
Ametangaza Rasmi msako wa kuondoa Makahaba Shinyanga
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amefanya kikao na Wazee, Machifu na Viongozi wa kidini mkoani humo, ili kujadiliana kwa pamoja kupeana ushauri, kuchota Nasaha zao pamoja na kujadili na kutatua changamoto ambazo zinawakabili wazee.
Kikao hicho kimefanyika leo Januari 24,2024 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho, amesema Serikali inawathamini Wazee, Machifu na Viongozi wa kidini katika kudumisha amani, kusimamia maadili ya vijana pamoja na kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya taifa, kutokana na kutoa ushauri mzuri kwa viongozi, ndiyo maana ameamua kukutana nao ili kujadiliana mambo mbalimbali pamoja na kuchota Nasaha zao.
“Nimekutana na nyie Wazee, Machifu na Viongozi wa dini ili kuchota Nasaha zenu kwa Maendeleo ya Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla, pia kujadiliana mambo mbalimbali ambayo yanawakabili na kuyatatua ili tuendelee kuwa enzi wazee wetu na kuwatunza chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan,”amesema Mndeme.
Mmomonyoko wa Maadili kwa vijana
Aidha, Mndeme amewaomba Wazee,Machifu na Viongozi wa dini kuisaidia pia Serikali kusimamia suala la Mmomonyoko wa maadili kwa vijana na malezi ili kuliokoa taifa pamoja na kuwakemea kuacha kutumika na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi ikiwamo kujiingiza kwenye Maandamano yasiyo na tija kwao, na kuiga mambo ya kigeni ikiwamo ushoga.
“Vijana msitumike kuwa chombo cha kuvuruga amani ya nchi, msikubali kutumia kwa maslahi ya watu binafsi na kujiingiza kwenye Maandamano yasiyo na tija kwenu, tuidumishe amani ambayo imeasisiwa na wazee wa taifa hili Amani Abeid Karume, Mwalimu Nyerere na sasa yupo Rais wetu Samia ana endelea kuidumisha, nawaombeni Wazee tuwasimamie vijana,”amesema Mndeme.
Msako Makahaba.
Amesema kutokana kusimamia suala la maadili kwa vijana, ametangaza Rasmi kuanzisha Oparation ondoa Makahaba Shinyanga, na kuzishughulikia nyumba za wageni ambazo zinafanya biashara ya ukahaba, ili kulinda maadili ya vijana.
“Natangaza kiama wale wote wanaofanya biashara ya kuuza miili yao waache, tunaanza msako kuanzia leo, bila kuchukua hatua watoto wetu watajifunza nini, wazee wangu na shukuru kwa kunipa Baraka hizi za kufanya Oparation ya Makahaba Shinyanga na washughulikia pamoja na nyumba za wageni ambazo zinafanya biashara hiyo ya ukahaba,”amesema Mndeme.
Suala la uandikishaji watoto shuleni.
Amewaomba pia wazee kuhimiza suala la uandikishaji watoto shuleni wa darasa la awali na la kwanza,pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shule takwimu ambazo zinaonyesha haziridhishi ili wahudhurie masomo na kupata elimu ambayo itatimiza ndoto zao.
Ametaja takwimu za uadikishaji wanafunzi wa darasa la awali kwamba maoteo kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka (2022) ilikuwa ni kuandikisha watoto 7,579 lakini wameandikishwa 39,831 sawa na asilimia 53, darasa la Kwanza Maoteo kuandikisha wanafunzi 69,792 lakini wameandikishwa 56,452.
Amesema kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza walioripoti shule hadi sasa ni 19,307 sawa na asilimia 50, lakini waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 38,570 na kuwaomba viongozi hao wahimizi wazazi kuwapekea shule watoto hao hata kama hawana Sare za Shule.
Kipindupindu.
Mndeme amewaomba pia wazee, machifu na viongozi hao wa dini waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuzingatia suala la usafi wa mazingira, pamoja na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kukabiliana na ugonjwa kipindupindu pamoja na kujenga vyoo bora na kuvitumia.
Amesema wagonjwa wa kipindipindu kwa Mkoa mzima wa Shinyanga wapo 139, wanaofuatiliwa ambao walikutana na wagonjwa kipindupindu 398 na walifariki na ugonjwa huo ni watu Sita.
Mipango ya Maendeleo.
Katika hatua nyingine Mndeme,amesema Serikali mkoani humo itaendelea kusimamia mipango ya maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwamo ya Afya, pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi, huku akiahidi kwamba katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, watasimamia sheria, kanuni na taratibu na utafanyika kwa Amani na utulivu.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano, akizungumza kwenye kikao hicho, wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwathamini wazee pamoja na Rais Samia na kutatua kero zao ikiwamo huduma ya Afya.
Nao baadhi ya wazee akiwamo Benard Itendele, akizungmzia suala la Mmomonyoko wa maaadili,amesema vijana wa siku hizi wamekuwa wakaidi na wakiitwa na wazee kupewa nasaha wamekuwa hawaitikii wito huo na kuwaona kama wamepitwa na wakati, huku akibainisha kwamba hawataka kata tamaa bali wataendelea kukemia Mmomonyoko huo wa maadili.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Hamisi, amesema suala la Mmomonyo wa maadili limekuwa kubwa hivyo ni vyema likakemewa pamoja na watoto kupewa elimu ya kiroho hasa katika siku za wikendi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Sheikh Balilusa Hamis akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza la ushauri Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akizungumza kwenye kikao hicho.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile akizungumza kwenye kikao hicho.
Wazee,Machifu na Viongozi wa dini wakiendelea na kikao.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Mkusanya akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Chifu Jidola Njange akichangia kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wazee wakichangia kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wazee wakichangia kwenye kikao hicho.
Wazee wakichagia kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wazee wakichangia kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464