MBUNGE WA KISHAPU BONIPHACE BUTONDO AWAFARIJI WAFIWA WALIOPOTEZA WATOTO WAO WAWILI KWA KUANGUKIWA NA NYUMBA
Watoto wawili wa familia Moja wamepoteza maisha kwa kuangukiwa na nyumba majira ya usiku katika Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Watoto hao ni Felister John aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza, na Razalo John Darasa la Sita, na mazishi yao yamefanyika leo, huku yakihudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu, Padri John Kinga, na Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo.
Butondo akizungumza na wananchi kwenye msiba huo, amewataka wananchi ambao wanaishi kwenye nyumba zisizo imara wasiishi kwenye nyumba hasa katika msimu huu wa mvua kubwa, pamoja na wale ambao wapo maeneo ya mabondeni ili kuepuka kutokea maafa vikiwamo vifo.
Amesema familia kuishi katika nyumba ambazo zimechoka ni hatari hasa katika msimu huu wa mvua kubwa, na hivyo kuwasihi watafute nyumba ambazo ni imara hata kuishi wa ndugu zao kwa muda ili kuepukana na maafa kama ilivvyo tokea katika Mji wa bwana John Stephano ambaye amepoteza watoto wake wawili kwa kuangukiwa nyumba kutokana na kuishi katika nyumba ambayo imechakaa.
"Nawasihi ndugu zangu msiishi katika nyumba ambazo zipo hoi ni bora mhame na wale ambao mnaishi mabondeni, ili kuepuka msipatwe na majanga,"amesema Butondo.
Amewataka pia wananchi wote katika Jimbo hilo la Kishapu, pia wajenge utamaduni wa kujenga nyumba ambazo ni imara na kuondokana na nyumba za Tembe,ambazo katika msimu huu wa mvua zinakuwa siyo imara na kuhatarisha maisha yao.
Aidha, kifo cha watoto hao wawili kimeelezwa kilitokea baada ya kuangukiwa na nyumba yao ya Tembe ambayo ilikuwa chakavu na na Kingo za nguzo zilikuwa zimeshaoza, na kwamba nyumba hiyo ilizidiwa mchanga uliokuwa umewekwa juu ya Tembe,na kisha kuanguka na kuwaponda watoto hao na kuwa umiza vibaya sehemu za vifuani na kupoteza maisha.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akishirikiana na wananchi wa Ukenyenge kuchimba Makaburi kwa ajili ya kuandaa nyumba za milele za watoto hao.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiendelea kushirikiana na wananchi kuchimba Makaburi mawili ya watoto hao ili kuwahifadhi katika nyumba za milele.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia) akibadilishana mawazo na Padri John Kinga wa Parokia ya Wila kwenye Msiba wa watoto hao.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akimfariji Mama wa watoto hao Bi Maria Charles na kumpa pole ya kuondokewa na watoto wake wawili.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiendelea kuwafariji wafiwa.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiangalia nyumba ambayo ilianguka na kusababisha vifo vya watoto hao.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi ambao wamefika kwenye Msiba huo na kutoa pole pamoja na kuwapatia Nasaha ya kuishi katika nyumba ambazo ni salama na imara hasa katika msimu huu wa mvua.