KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO KISHAPU IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Kamati ya fedha na mipango robo ya pili mwaka wa fedha 2023/2024 ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Kilimo na Afya yenye thamani ya Shilingi 623,488,417.06.

Ziara ya kamati ya fedha na mipango chini ya Mwenyekiti wake Mhe. William Jijimya imeridhishwa na Miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali

Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri kwa niaba ya kamati amesema kwamba kwa miradi yote waliyopita kukagua ipo katika hari ya ubora
"Miradi yote tuliyoikagua leo ipo katika hari ya ubora hivyo tunampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji na timu yake kwa usimamizi mzuri wa miradi kuhakikisha miradi inakwenda vizuri licha ya changamoto ndogondogo miradi ipo Vizuri wataalamu waendelee kusimamia ili kuboresha zaidi" amesema Jijimya

Kwa upande wake Richard Dominick ambaye ni Diwani wa kata ya Talaga amepongeza Mkurugenzi kwa kuhakikisha Miradi inayotekelezwa wanachi wanahusishwa kwa ukaribu sana kwa sababu inakuwa rahisi kufuatilia utekelezaji wake.
Naye Mhe. Joel Ndettoson ametoa rai kwa Wananchi ambao miradi inatekelezwa kwenye maeneo kuwa na uchungu nayo kwani fedha nyingi sana zinatumika kwaajilinya ujenzi wa Miradi hiyo.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu ameipongeza Sana Serikali ya awamunya Sita Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiamini Kishapu kuiletea fedha nyingi kwaajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464