RAIS SAMIA AMETOA ZAWADI KITUO CHA WATOTO YATIMA SHINYANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwa watoto Yatima ambao wanalelewa katika Kituo cha Shinyanga Society For Ophans kilichopo Bushushu Manispaa ya Shinyanga.
Zawadi hizo zimekabidhiwa leo Januari 4, 2024 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme kwa niaba ya Rais Samia.
Samizi akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo amesema Serikali ipo bega kwa began a wadau wa maendeleo ambao wamekuwa wakisaidia watoto hao Yatima kwa kuwapatia huduma ya malezi pamoja na elimu.
“Rais Samia hua anautaratibu wake kila sikukuu lazima awashike mkono watoto Yatima na wale ambao wanaishi katika Mazingira hatarishi, na katika kituo hiki ametoa zawadi ya Mchele, Sukari,Mafuta ya kupikia, Nguo pamoja na Juice,”amesema Samizi.
Watoto hao Yatima akiwamo Hadija Ally, wamemshukuru Rais Samia kwa kuwapatia zawadi hizo, na kuahidi wataendelea kumuombea kwa Mungu ili aendelea kuwa na Afya njema ili awatumikie watanzania na kuwasaidia watoto Yatima.
Naye Meneja wa Kituo hicho cha watoto Yatima Farhiya Said, ameshukuru kwa zawadi hizo, na kuipongeza Serikali kwa kuwaunga mkono, huku akiahidi wataendelea kuwapa watoto hao malezi bora pamoja na elimu, na kubainisha kwamba wana watoto 35, wanasoma Shule za msingi 26 na Sekondari 9.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akikabidhi zawadi kwa watoto Yatima ambazo zimetolewa na Rais Samia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiendelea kukabidhi zawadi kwa watoto Yatima ambazo zimetolewa na Rais Samia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiendelea kukabidhi zawadi kwa watoto Yatima ambazo zimetolewa na Rais Samia.
Zoezi la kukabidhi zawadi likiendelea.
Zawadi zikishushwa kwenye gari.
Zawadi zikiendelea kushushwa kwenye gari.
Zawadi zikiendelea kushushwa kwenye gari.
Muonekano wa zawadi.
Zawadi zikiendelea kushushwa kwenye gari.