MKUU WA WILAYA YA KISHAPU JOSEPH MKUDE AMEONGOZA WANANCHI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KUKABILIANA NA UGONJWA KIPINDUPINDU

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Joseph Modest Mkude ameongoza wananchi wa wilaya hiyo kufanya Usafi wa Mazingira kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Shughuli za usafi wa mazingira leo Januari 20, 2024 ambapo zilianzia eneo la soko la wajasiliamali kata ya Kishapu ambapo wananchi nawatumishi wa taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Halmashauri walifanya usafi katika mitaro ya barabara, maeneo ya taasisi na Maeneo ya mnadani nakumalizia kwa kufanya usafi katika eneo la dampo.
Mhe. Mkude amewataka Wananchi wajijengee tabia ya kufanya usafi Mara kwa Mara iwe tabia ya kudumu kwa wananchi kuwa wasafi pamoja na mazingira yanayowazunguka.

"Niwashukuru sana Wananchi pamoja na Wanafunzi mliojolitokeza leo kwenye usafi Kuna muda tunachukulia jambo hili la usafi kama la haraka jambo la usafi inatakiwa liwe jambo endelevu Wananchi wote inatakiwa waje ngewe uwezo wa kuwa wasafi kama Vile ambavyo anafanya Mkurugenzi anachukua wanafunzi anawajengea tabia ya kuwa wasafi hii itasaidia Wananchi kutunza Mazingira na Kuwa wasafi katika maeneo yao." Amesema Mkude.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson amesema kwamba suala la Usafi liwe utamaduni na isiwe msimu wa Kipindupindu tu. na kwa upande wa Halmashauri wamejipanga kuleta mtambo kwa ajili ya kuchimba shimo la taka ili iwe rahisi kuthibiti taka, pia Halmashauri imetenga eneo kubwa la Dampo ambalo litakuwa ni Dampo kubwa la Kishapu litahudumia wananchi wote kwa kukusanya taka na kupelekwa katika dampo hilo, Wananchi watashiriki kulipa gharama za kujusanyia Uchafu.

Naye Afisa Afya wilaya ya Kishapu Ndugu. Godfrey Kisusi amesema kwamba Wamejipanga kikamilifu kudhibiti Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa Mara kwa mara kwa wananchi pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na Kipindupindu.

Aidha Mhe. Mkude amesema kwamba Kuna maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kuweka uchafu na siyo kila sehemu na matangazo ya kuweka uchafu yatotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464