DC APIGA MARUFUKU BIASHARA YA CHAKULA MASHULENI ILI KUEPUKANA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini

Suzy Butondo,Shinyanga press blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi amepiga marufuku biashara yeyote ya chakula mashuleni kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu kuendelea kuwepo katika manispaa ya Shinyanga.ambapo manispaa wamegundulika wagonjwa tisa nane wameruhusiwa mmoja anaendelea kuhudumiwa.

Tamko hilo amelitoa leo wakati akizungumza kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga mjini kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga, ambapo amepiga marufuku biashara yoyote ya chakula mashuleni.

"Nimetoa tamko hili kwa sababu katika chuo cha Shycom iliyoko mjini hapa kuna wagonjwa wametokea hapo,ndiyo maana napiga marufuku hata kwenye shule zingine nisione biashara ya chakula ikiendelea, kwani hali ni mbaya sihitaji chakula kutoka nje tuvumiliane tu, badala yake wazazi wachangie chakula mashuleni ,"amesema Samizi.

Amesema mgonjwa wa kwanza alitokea Kishapu, hivyo amewaomba madiwani wawahimize wananchi wachemshe maji wafanye usafi watumie chakula cha moto katika maeneo yao na wasiruhusu chakula kiuzwe mashuleni wawahamasishe wazazi wachange fedha ili wapikiwe chakula cha moto mashuleni 

"Pia niwaomba sana waheshimiwa madiwani turudi tukahamasihe watoto wote waliofaulu waende shuleni itakuwa hakuna maana ya ujenzi wa shule tushirikiane tuwahamasishe, Rais wetu ametoa fedha nyingi sana za kujenga shule ili watoto wote wasome tena bure kabisa, hivyo tuhimizane ili watoto wote waliofaulu na wanaostahili kuandikishwa waende shule hata kama hana sare za shule aende tu"amesema Samizi.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amewataka watoto wote waliofaulu kidato cha kwanza waende shuleni,na wanaoandikishwa darasa la awali na la kwanza waende shule, kwani mpaka sasa shule mpya ya Butengwa iliyoko mjini hapa waliochaguliwa ni 361 waliochukua form ni 266 walioingia shuleni ni 132 hivyo ni vizuri wazazi wawahimize watoto waende shule.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Anord Makombe amewahimiza viongozi wote wa kata kuhakikisha wanachama wote wanajisajili na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili kujiandaa na uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa, na viongozi wote wa kata na matawi wafanye kazi kwa bidii ili kuhakikisha CCM inasonga mbele, ikiwa ni pamoja na kutatua kero mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe akizungumza kwenye kikao cha halmashauri kuu Wilaya ya Shinyanga mjini 
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe akizungumza kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Wilaya ya Shinyanga mjini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mjini Johari Samizi katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Jonathan Madete akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu

Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Shinyanga mjini  James Jumbe akiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu cha wilaya ya Shinyanga 
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya wakiwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Shinyanga mjini
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464