KANISA LA PHILADEFIA LATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE UHITAJI NDEMBEZI




Suzy Butondo, Shinyanga pres blog

Kanisa la Philadelfia Miracle Temple lilikoko kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga limetoa msaada wa mashati Dafutari, kalamu na rula zenye thamani ya zaidi ya 300,000 kwa watoto wahitaji wanaoishi katika kata ya Ndembezi mtaa wa Butengwa manispaa ya Shinyanga Mkoani hapa.

Akikabidhi msaada huo mchungaji msaidizi wa Kanisa hilo Hanania Clement amesema kanisa la Philadelfia linatoa msaada huo kwa watoto ili kuwafanya watoto hao wasome kwa bidii na wakulie kwenye mazingira mazuri na maadili mema ya kumpendeza Mungu.

"Lengo letu ni kuitengeneza jamii ikulie kwenye mazingira mazuri wasijisikie vibaya wajione wako sawa na watoto wenzao ambao wana uwezo, na hii ni awamu ya tatu toka kanisa lianze kutoa msaada kwa wahitaji hawa, tunaamini siku nyingine tutawasaidia zaidi jinsi Mungu atakavyotuwezesha,"alisema Hanania.

"Pia niwaombe wazazi watoto hawa mnatakiwa muwalee katika maadili mema, msiwaruhusu watoto kwenda kwenye majumba ya starehe nyakati za sikukuu, kwani wanapoenda huko wanajifunza mambo ambayo si ya kimaadili, na anapoendelea kukua ana kuwa na mazoea ya kwenda huko,"alisema Hanania.

Herman Hezron ambaye ni mchungaji saidizi wa kanisa hilo amewataka watoto hao ambao wamepatiwa msaada huo wasome kwa bidii ili baadae waweze kutimiza ndoto za maisha yao wasijiingize kwenye vikundi visivyo na maadili mema.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Philadelfia Miracle temple Baraka Laizer amesema kwa upendo mkubwa kanisa lake limeanzisha huduma ya kusaidia wahitaji kila mwaka vifaa mbalimbali vya shule, kwani kuna wakati inapofika wakati wa kwenda shule watoto wanakuwa hawana vifaa vya shule kama sare za shule na madaftari hivyo kanisa linawasaidia.

"Mpaka sasa tuna wahitaji 24, tulianza na watoto 21 lakini wanaongezeka kuanzia watoto wa chekechea shule za msingi na sekondari tunatoa vifaa vya shule jinsi Mungu anavyotuwezesha, niwaombe na wadau wengine wenye moyo wa upendo tuwasaidie watoto hawa kwani bado wana uhitaji mkubwa ikiwemo chakula godoro kuwapelekea wanakoishi karibuni sana"amesema Laizer.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Butengwa Onesmo Mahenda amelishukru kanisa kwa kuendelea kuisaidia jamii ya Mtaa wake,hivyo amewataka watoto watumie vifaa hivyo vizuri na wasome kwa bidii ili waweze kufaulu vizuri na kuweza kutimiza ndoto zao,
Pia amewashukuru wazazi kwa kuwaleta watoto hao kuja kupata vifaa vya shule na kuwataka wazazi na walezi wawahimize watoto waweze kupenda shule na wahudhulie masomo yote.

"Nilishukuru kanisa hili kwa kujitoa pale mlipotoa Mungu akawaongezee, naomba sana wazazi mjitahidi kuhamasisha watoto hawa waweze kupenda shule na muwalee katika mazingira ya kupenda shule msiwaachie kwenda kwenye miziki ya kidunia muwafundishe maadili mema ya kidini afadhali waende kwenye disco la kimungu kuliko kuwapoteza"amesema Mwenyekiti Mahenda

Baadhi ya wazazi akiwemo Maria Joseph ameshukru msaada huo uliotolewa na kanisa na kuwataka waendelee na moyo huo huo, kwani huo ni upendo wa pekee kujitolea kwa ajili ya wengine wenye uhitaji na Mungu atawabariki.
Mchungaji msaidizi wa kanisa la Philadelfia miracle Temple Hanania Clement akiwagawia watoto wahitaji vifaa mbalimbali vya shule

Watoto wakiwa na viongozi mbalimbali wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple baada ya kuwagawia vifaa mbalimbali vya shule

Watoto wakiwa na viongozi mbalimbali wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple baada ya kuwagawia vifaa mbalimbali vya shule
Watoto wakiwa na viongozi mbalimbali wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple baada ya kuwagawia vifaa mbalimbali vya shule
Watoto wakiwa na madaftari baada ya kugawiwa
Watoto wakigawiwa vifaa mbalimbali vya shule
Baadhi ya watoto wakisubiri kugawiwa vifaambalimbali vya shule vilivyotolewa na kanisa la filadelfia Miracle Temple



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464