Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba amekabidhi zawadi awamu ya nne inayoishia Desemba 2023 kwa Washindi wa Chemsha Bongo na Salome Makamba ambayo inaendeshwa na Kituo cha Matangazo Redio Faraja Fm Stereo.
Miongoni mwa waliokabidhiwa zawadi ni pamoja na washindi 32 wa majiko ya Gesi, Washindi wa nyongeza ya mtaji isiyokuwa na riba wala marejesho kwa makundi maalum ya wanawake, vijana, wazee na wenye ulemavu, zawadi za Jezi na mpira wa miguu kwa timu 9 za mpira na vifaa vya shule kwa wanafunzi.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi imefanyika leo Ijumaa Januari 26,2024 katika uwanja wa Redio Faraja mjini Shinyanga na tahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo na masuala ya kijamii wakiwemo viongozi wa Serikali, taasisi za Serikali na binafsi.
Meneja vipindi wa Redio Faraja na Mratibu wa Chemsha Bongo na Salome Makamba, Simeo Makoba ameeleza kuwa Redio Faraja kupitia Falsafa yake ya ‘Tunajenga Jamii’, imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na kwa karibu na wadau wengine ikiwemo serikali kuhakikisha jamii nzima inaishi kwa usalama, furaha, umoja, upendo, amani na mshikamano.
“Chemsha Bongo na Salome Makamba licha ya kuwawezesha wananchi kushinda zawadi mbalimbali, imelenga kuwapa msukumo wa kutafuta na kufuatilia taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya kijamii ikiwemo mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali, kuibua vipaji kupitia michezo pamoja kuvijengea uwezo wa kiuchumi vikundi vya wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu”,amesema Makoba.
Amesema Programu hiyo inavijengea uwezo wa kiuchumi vikundi vya wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu ambavyo vinakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa mitaji na wakati mwingine kulazimika kuchukua mikopo isiyokuwana tija, yenye masharti magumu ambayo badala ya kuwasaidia imeongeza ukali wa maisha kutokana na kuhangaika usiku na mchana wakitafuta marejesho.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Makamba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwa kufungua fursa za uchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi.
“Niliahidi kuwa nataka kusisimua maendeleo mkoa wa Shinyanga, hapa hakuna biashara ya itikadi, tuna biashara ya maendeleo katika mkoa wa Shinyanga, Hatuongelei vyama hapa tunaongelea wivu wa maendeleo”,amesema Mhe. Makamba.
“Leo tunakabidhi zawadi kwa washindi wa Chemsha Bongo na Salome Makamba lakini pia nimekabidhi cherehani na shilingi 300,000/= kwa dada yetu Zawia Ibrahim ili kumsaidia kukabiliana na changamoto za kiuchumi anazokumbana nazo. Napenda kuwataarifu kuwa Programu ya Chemsha Bongo na Salome bado inaendelea”,amesema Makamba.
Mbunge huyo wa Viti maalum amewataka Wanawake na Vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024.
“Wanawake na vijana hakikisheni mnaingia kwenye ngazi za maamuzi, hakikisheni mnaogombea nafasi za uongozi, tunataka usawa wa kijinsia asilimia 50% kwa 50%”,ameongeza.
Katika hatua nyingine amesema bado changamoto ya ukatili wa kijinsia ipo katika jamii hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutoa taarifa za matukio ya ukatili badala ya kuyanyamazia.
“Matukio ya ukatili bado yapo katika jamii.Pia kuna ukatili unaendelea ndani ya ndoa, mme wako au mke wako anakufanyia ukatili halafu halafu unanyamaza, ni jukumu letu sote kuwa mabalozi wa amani na tuwe mabalozi wa maendeleo, suala la ukatili haliangalii chama wala itikadi lazima sote tulipinge”,amesema.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Redio Faraja, Anikazi Kumbemba amesema Programu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba inasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda watoto na kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Tunamshukuru Mhe. Salome kwa kuendelea kuwezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapatia mitaji isiyo na riba, kusaidia vifaa vya michezo kwa vijana. Majiko haya yaliyotolewa na Mhe. Salome Makamba yatasaidia sana kupunguza ukataji miti ili kulinda mazingira. Msiende kuyauza, yatunzeni kwa ajili ya kutunza mazingira”,amesema Kumbemba.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Fraterine Tesha ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga na Mkuu wa Dawati na Jinsia na Watoto Monica Sahere wamemshukuru na kumpongeza Mbunge Salome Makamba kwa namna anavyoshirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Redio Faraja kuzuia vitendo vya uhalifu.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akizungumza wakati akikabidhi zawadi kwa Washindi wa Chemsha Bongo na Salome Makamba ambayo inaendeshwa na Kituo cha Matangazo Redio Faraja Fm Stereo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Redio Faraja, Anikazi Kumbemba akizungumza wakati wa hafla hiyo

Meneja vipindi wa Redio Faraja na Mratibu wa Chemsha Bongo na Salome Makamba, Simeo Makoba akizungumza wakati wa hafla hiyo

Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Fraterine Tesha ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa Dawati na Jinsia na Watoto Monica Sahere akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha wajasiriamali
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha watu wenye ulemavu
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha Wanawake wajasiriamali
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha wanawake na wanaume wajasiriamali
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha Wanawake cha wanawake wajasiriamali
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha watu wenye ulemavu
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya madaftari na taulo laini kwa mwanafunzi mshindi wa awamu ya nne ya Chemsha bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya madaftari kwa mwanafunzi mshindi wa awamu ya nne ya Chemsha bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jezi na mipira kwa moja ya Timu washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mmoja wa washindi wa awamu ya nne ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464