Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rebeca Machiya (36) mkazi wa mtaa wa Mwasele B kata ya Kishapu Wilayani humo Mkoani Shinyanga amekutwa amefariki ndani ya chumba chake, huku akiwa amenyofolewa macho, matiti, na sehemu za siri,
Kufuatia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka waganga wote wa jadi wilaya ya Kishapu kufanya uchunguzi wa haraka ili kuhakikisha viungo hivyo vimepatikana.
Mkude akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya Kishapu amesema jeshi la polisi Kishapu liligundua tukio hilo Januari 30, 2024 ambapo amewaomba waganga wa tiba asili kutoa ushirikiano ili kuhakikisha viungo vya marehemu huyo vinapatikana kwa wakati.
"Nimeona niwaite waganga wote wa jadi katika kikao hiki ili niweze kuwashirikisha suala hili, kwani kifo cha mama huyu ni cha aibu sana niwaombe waganga wa jadi tushirikiane kwa pamoja ili viuongo vya huyu mama vipatikane, kwani ni jambo la aibu sana, kuna watu wanafikiri kufanya hivyo ni kutajirika, huwezi kutajirika kwa kunyofoa viungo vya binadamu niwaombe mtoe ushirikiano wa haraka "amesema Mkude.
Mkude amewaomba viongozi wa dini waendelee kuhubiri ili kudumisha amani, na madiwani waendelee kukemea jambo hilo ili lisije kuendelea kujitokeza katika wilaya ya Kishapu na Mkoa wa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa waganga wa tiba asili wilaya ya Kishapu Ndembi Seni Mabeshi amesema waliofanya kitendo hicho ni watu tu ambao wana masilahi yao siyo waganga wa jadi, hivyo wameahidi kufanya uchunguzi ili kuweza kuwabaini waliofanya tukio hilo.
Diwani wa kata ya Uchunga Mshini Masunga ambaye naye ni mganga wa jadi akizungumza kwenye baraza la madiwani kwa niaba ya waganga amesema amepokea kwa masikitiko sana tukio la kifo cha mwanamke huyo, kwani aliyefanya mauwaji hayo ana roho mbaya, analaani na anakemea tabia hiyo isijitokeze tena
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson amesema mazingira haya si ya kimapenzi ni ya kishirikina kuna baadhi ya watu wanaamini watapata utajili wa hivyo lakini huwezi kulinganisha na uhai wa mtu, hivyo inatakiwa kupambana ili upate maendeleo, hivyo kinahitajika ushirikiano ili kupata ushahidi kwa siri.
Kwa upande wake mwernyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu amewaomba waganga wa jadi walifuatilie ili warudishe viungo hivyo " kwani huu ni ushenzi usiokaribu na Mungu, tulifuatilie na tumbaini aliyefanya hivyo, na miwaombe wana kishapu tulinde watu wetu, tuwajue wageni wanaotutembelea kwenye maeneo yetu"amesema.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya amewaomba madiwani kukemea suala hilo, ili lisiendelee kujitokeza kwani ni aibu kubwa kutokea kwa tukio hilo, hivyo wanganga watoe ushirikiano ili liweze kutokomezwa tukio hilo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani
Mwenyekiti wa waganga wa tiba asili wilaya ya Kishapu Ndembi Seni Mabeshi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Kishapu
Diwani wa kata ya Kishapu Joel Ndetoson akizungumzia tukio hilo kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya kishapu
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Kishapu