MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA SHINYANGA AWAFUNDA VIONGOZI WA CCM KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya wazazi na chama kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM

Suzy Butondo, Shinyanga Press blog

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi amewataka viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa wabunifu, kufanya kazi kwa kufuata kanuni na kuzingatia maadili ya uongozi, ikiwa ni pamoja na kukemea ukatili na kuwafundisha maadili mema watoto.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, yaliyofanyika kimkoa Shinyanga mjini katika kata ya Ndala, ambapo amesema viongozi wote wa jumuiya na chama wafanye kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria ikiwa ni pamoja na kukemea ukatili wa aina mbalimbali na kuwafundisha maadili mema Watoto wao.

Siagi amesema kiongozi yeyote anatakiwa kuwa na maadili mema, na awe na uvumilivu na staa, hatakiwi kutumia nguvu ya hoja, awe tayari kujikosoa, hivyo anatakiwa aongoze kwa dira na apende kufanya kazi na kuwa na imani na watu anaowaongoza na kujitolea kufanya kazi, bila kusahau kukemea tabia za kikatili zinazoendelea kufanywa na baadhi ya watu .

Aidha amewataka wazazi kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwalea watoto katika maadili mema ili wasijiingize kwenye vitendo visivyo na maadili yasiyofaa.

"Kazi ya kiongozi ni kuwatumikia wananchi, kusikiliza kero za wananchi hivyo tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii bila kumbagua mtu yeyote , tupendane tuendelee kudumisha amani huku tukemee vitendo vya ukatili tuwafundishe watoto wetu maadili mema, tuzungumze na watoto wetu wabadilike wawe na tabia njema"amesema Siagi.

Pia amewataka wananchi wote kuchukue tahadhari kujikinga na kipindu pindu wanawe mikono, kwa sabuni na maji tiririka na wale chakula cha moto ilikujikinga naugonjwa wa kipindu pindu.

Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Shinyanga Agness Kahabi amewaomba viongozi wote kukienzi chama cha mapinduzi, kwani toka kianzishwe tarehe 5,2,1977 kinaendelea kuwa kwenye Dola, hivyo amewataka viongozi wasiteteleke.

Katibu wa wazazi wilaya ya Shinysnga Doris Kibabi pia ameshauri wazazi wote kuwapeleka watoto wote waliofaulu kidato cha kwanza shule ili wasipitwe na vipindi vya masomo ambayo tayari walimu walimu wameshaanza kufundisha ikiwa ni pamoja na kuwakemea wasiige vitendo vya uovu visivyofaa.

Mwenyekiti wa Chipukizi Mkoa wa Shinyanga Maimuna Saidi amewaasa wazazi wasiwafungie ndani wanafunzi waliofaulu kwa kigezo cha kukosa sare za shule badala yake wawanunulie madaftari na kalamu waende shule kwaajili ya kuanzamasomo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya wazazi na chama kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya wazazi na chama kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji wazazi Mkoa Agnes Kahabi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mjumbe wa kamati ya Uchumi Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Mery Izengo akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Katibu malezi na mazingira Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Richard Mseti akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mjumbe wa kamati ya Uchumi Piter Frank akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa UvccmWilaya ya Shinyanga Jonathan Madete akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa Chipukizi Mkoa wa Shinyanga Maimuna Saidi akizungumza.kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Diwani wa Kata ya Masekelo Zamda Shabani akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Kishapu akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mtendaji wa kata ya Ndala akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Kishapu akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ndala akizungumza Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Kishapu akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Kishapu akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM

Katibu muenezi wa kata ya Ndala akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa wazazi kata ya Ndala Mariam
akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Viongozi wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM

Viongozi wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya. kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Viongozi wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya. kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM

Viongozi wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwakwa Chama Cha Mapinduzi CCM

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464