NAIBU WAZIRI KATAMBI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA KUZALIWA KWA CCM, AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana na ajira akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa CCM

Suzy Butondo, Shinyanga Press blog

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana na ajira,ameahidi kuzishughulikia changamoto zote zilizopo katika jimbo la Shinyanga .

Ahadi hiyo ameitoa leo kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa chama cha mapinduzi CCM yaliyofanyika kimkoa kata ya Ndala wilaya ya Shinyanga mjini, ambapo amesema serikali ya mama samia kazi yake ni kuleta fedha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

" Kwa kipindi kifupi tumefanya maendeleo makubwa lakini hizi changamoto ndogo tutaenda kuzitatua, Ibinzamata tutaweka kivuko, daraja la upongoji tutatengeneza kubwa ili gari ziweze kupita na kupishana, Pia na kwenye kata zingine za manispaa tutaendelea kuzifanyia kazi " amesema Katambi.

"Mikopo ya halmashauri tutaendelea kuitoa ili wananchi waendelee kujikwamua kiuchumi, pia tunahakikisha miradi inatekelezwa vizuri tena kwa kiwango kikubwa, pia niwakumbushe tarehe 28 wananchi wote tujitokeze kwa wingi, tuje tusikilize ujumbe aliopewa na mheshimiwa Rais na sisi tumpe ya kwetu ili akayafanyie kazi"amesema Katambi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wazazi MkoaJonh Siagi akiwa kwenye viwanja vya kata ya Ndala amesema tunapoadhimisha maadhimisho haya tunaeleza mafanikio yaliyofanyika, kwani Rais ameendelea kumimina fedha nyingi kuanzia kwenye kata hadi mikoa, amegusa kwenye sekta mbalimbali,,amesema Siagi.

"Sisi katika uchaguzi uliopita hatukukosea kuchagua madiwani, wabunge, ndiyo maana tunaona maendeleo yanafanyika masoko yetu yanaendelea kutengenezwa kutokana na fedha nyingi za maendeleo,

"Niwaombe kina mama pale zitakapotangazwa fedha za halmashauri tuchangamkie fursa ili tuweze kujikwamua kiuchumi, fedha zipo za kutosha ila tukumbuke kurejesha ili tuweze kupata zaidi, pia niwaombe wananchi tujitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili tuchague viongozi wanaofaa"amesema Siagi

Aidha katika maadhimisho hayo Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban amekabidhi jezi na mipira miwili kwa timu mbili za mpira alizozianzisha za kutoka Tawi A na tawi B katika kata hiyo ambapo yatahitimishwa tarehe 5,2,2024, ambapo watapewa zawadi washindi watakaoshinda
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa CCM
Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mkoa Rejina Ndulu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa CCM
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga
akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa CCM
Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mkoa Rejina Ndulu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuanzishwa kwa CCM
Diwani viti maalumu wa Shinyanga mjini Moshi Kanji akiwa kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa CCM yaliyofanyika kata ya Ndala Shinyanga mjini
Viongozi mbalimbali na wanachama wa Chama cha mapinduzi CCMwakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa CCM yaliyofanyika kata ya Ndala Shinyanga mjini

Katibu wa Wazazi Mkoa Rejina Ndulu akiwa na atibu wa wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi kushoto wakiwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji WazazibMkoa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi akikabidhi vifaa vya michezo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Jonh Siagi akikabidhi vifaa vya michezo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464