Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa zawadi za madaftari na kalamu kwa watoto wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kwa mara ya kwanza
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewataka wazazi ambao hawajapeleka kuwaandikisha watoto shuleni wawapeleke kuwaandikisha ili waweze kuanza masomo kwa pamoja na kuyajua mazingira ya shule yalivyo.
Agizo hilo amelitoa leo wakati akikagua wanafunzi wa shule ya awali na msingi katika shule ya Mwenge, Ngokolo seko dari na Butengwa shule ya sekondari ya wasichana iliyoko manispaa ya Shinyanga Mkoani hapa, ambapo amewataka wazazi wote wenye watoto wenye sifa ya kuandikishwa wawapeleke shuleni wakaandikishwe.
Mndeme amesema Rais Samia Suluhu ameshalipa ada, hivyo watoto wote watasoma bure hakuna wa kulipa ada, hivyo wazazi wote wanatakiwa wawapeleke watoto wao shuleni kwa ajili ya kuanza masomo kwa wakati na pamoja.
"Niwaombe wazazi ambao hawajawaleta watoto wao shuleni wawalete shuleni kwani shule tayari zimefunguliwa leo, madarasa yapo walimu wapo haiwezekani shule imeanza leo na watoto 79 katika shule ya Ngokolo, leteni watoto shuleni kuendelea kuwaacha nyumbani ni kumkosesha vipindi mtoto, kesho niombe wanafunzi wote waje mashuleni"amesema Mndeme
Pia amewataka wanafunzi wote kujiepusha na mambo yasiyo faa ya uovu badala yake wasome kwa bidii wamshike elimu asiende zake anaetaka kuwa daktari au kazi yeyoyote asoma vizuri awatii walimu wake ili waweze kupata elimu bora.
"Niwapongeze sana walimu kwakuendelea kusimia vizuri zoezi hili zoezi la uandikishaji na kukaribisha watoto na kuweza kuandikisha ili watoto waweze kuendelea na masomo yao kama kawaida"amesema Mndeme.
Kwa upande wake afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako amesema matarajio ya uandikishaji kwa darasa la kwanza na elimu ya awali yametokana na sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 awali walikuwa ni 75079 na mpaka sasa wameandikisha wanafunzi 47147 sawa na asilimia 62.
Kwa darasa la kwanza kwa mujibu wa sensa ni wanafunzi 69792 lakini mpaka sasa wameandikisha wanafunzi 44,432 sawa na asilimia 64, katika kidato cha kwanza wanafunzi 38963 wamefauli, hivyo wanatategemea kupokea taarifa mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali ya shule katika mkoa wa Shinyanga ambapo katika shule ya Ngokolo sekondari iliyoko manispaa ya Shinyanga tayari wanafunzi 79 wameripoti shuleni.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Ngokolo James Msimba amesema tayari wameshapokea wanafunzi 79 wa kidato cha kwanza na wwazazi wanaendelea kuijia fomu kwa ajili ya kujaza hivyo tunaendelea kupokea wanafunzi kuanzia leo.
Baadhi ya wazazi waliopeleka watoto wao katika shule ya awali na msingi Mwenge Emmanuel Msengi na Weru Staili wamesema wanawashukiru walimu kwa kuwapokea vizuri lakini kuna changamoto ya madarasa inaonekana wanafunzi ni wengi wanabanana darasani, hivyo wameiomba serikali iwaongezee madarasa ili waweze kudoma kwa uhuru watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa zawadi za madaftari na kalamu kwa watoto wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kwa mara ya kwanza
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa zawadi za madaftari na kalamu kwa watoto wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kwa mara ya kwanza
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa zawadi za madaftari na kalamu kwa watoto wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kwa mara ya kwanza
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mwenge baada ya kukagua daftari la kuandikisha wanafunzi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kwa mara ya kwanza Ngokolo manispaa ya Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto wa darasa la awali katika shule ya Mwenge
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na wqnafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mwenge
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua daftari la kuandikishaia wanafunzi wanaoanza awalina darasa la kwanza
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kwa mara ya kwanza Ngokolo manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na wanafunzi kidato cha kwanza shule ya wasichana Butengwa manispaa ya Shinyanga