WAATHIRIKA BWAWA LA MAJITOPE MGODI WA ALMASI MWADUI WAKABIDHIWA RASMI NYUMBA ZAO

Waathirika wa bwawa la Majitope Mgodi wa Almasi Mwadui wakabidhiwa nyumba zao

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,amezindua na kukabidhi nyumba 42 kwa Waathirika wa bwawa la Majitope Mgodi wa Almasi Mwadui ambao walipoteza makazi yao, mara baada ya bwawa hilo kupasuka na kuleta athari kwa wananchi.
Zoezi hilo la uzinduzi na kukabidhi nyumba hizo kwa wananchi limefanyika leo Februari 2,2024 Mahali ambapo zimejengwa baadhi ya nyumba hizo katika Kijiji cha Mwang'holo Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu.

Mndeme akizungumza wakati wa kuzindua na kukabidhi nyumba hizo, ameushukuru Mgodi wa Mwadui kwa kutekeleza Maagizo yote ya Serikali ya ulipaji fidia wananchi, na leo amekabidhi nyumba Rasmi kwa Waathirika ambao walisalia kulipwa fidia zao kwa kujengewa nyumba.
"Nawaombeni wananchi nyumba hizi ambazo tumezindua leo na kuwakabidhi, zitunzeni pamoja na kupanda miti, Serikali yenu inawathamini sana na imesimamia zoezi hili la ulipwaji fidia na sasa mnaishi katika nyumba bora na imara na kutoka kwenye Tembe," amesema Mndeme.

Aidha,amesema kwa wale wananchi Wanne ambao wamegoma kujengwa nyumba wakitaka walipwe pesa, amesema Serikali haina pingamizi bali watapewa pesa zao kwa kufuata utaratibu.
Katika hatua nyingine amewaagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu pamoja na TANESCO, kupeleka huduma hizo haraka kwenye nyumba hizo,ili kuboresha maisha bora kwa wananchi hao.

Meneja Mahusiano Mgodi wa Mwadui Bernard Mihayo,akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo, amesema Waathirika 47 ndiyo walipoteza nyumba zao huku wakimsaidia pia ujenzi wa nyumba Mwananchi ambaye alikuwa hajiwezi na hivyo kutakiwa kujenga nyumba 48.
Amesema Mpaka sasa wameshajenga nyumba 42 ambazo tayari zimekamilika na wananchi wanaishi,huku nyumba Mbili zikiendelea kujengwa na zipo hatua za renta, na wananchi hao wamechelewa kujengewa sababu awali waligoma.

Amesema kwa wale wananchi Wanne ambao wamegoma kujengewa nyumba zao tararibu na mazungumzo zinaendelea ili kulipwa pesa zao.
Amesema pia hatua ambayo inafuata kwa sasa ni kuhamisha Makaburi 14 ya Waathirika pamoja na kuwa anzishia miradi ya kuwaboresha vipato ikiwamo ufugaji Kuku na Mbuzi.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamekabidhi nyumba hizo akiwamo Samweli Kulwa, wameishukuru Serikali pamoja na Mgodi wa Mwadui kwa kuwajengea nyumba hizo na sasa wanaishi katika makazi imara.
Novemba 7 mwaka juzi 2022 Bwa la Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu lilibomoka na kisha tope kwenda kwenye makazi ya watu na kuleta madhara mablimbali lakini hapakutokea kifo, na hadi sasa wananchi wameshalipwa fidia zao na leo wamekabidhiwa nyumba.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi nyumba hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akionyesha Mchoro wa nyumba za awali ambazo walikuwa nazo wananchi na nyumba mpya ambazo wamejengewa na Mgodi kwa kulipwa fidia.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba hizo Waathirika wa Majitope la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi nyumba.
Diwani wa Mwadui Luhumbo Francis Manyanda akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi nyumba.
Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizundua nyumba hizo na kuzikabidhi kwa Waathirika wa tope la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na zoezi la uzinduzi wa nyumba hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na zoezi la uzinduzi wa nyumba hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na zoezi la uzinduzi wa nyumba hizo.
Muonekano wa nyumba ambazo Waathirika wa bwawa la Majitope wamejengewa na Mgodi wa Almasi Mwadui kwa kulipwa fidia.
Muonekano wa nyumba ambazo Waathirika wa bwawa la Majitope wamejengewa na Mgodi wa Almasi Mwadui kwa kulipwa fidia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipanda Mti mara baada ya kumaliza kuzindua na kukabidhi nyumba hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika nyumba ambazo wamejengewa Waathirika wa tope la Mgodi wa Almasi Mwadui kwa kulipwa fidia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme awali akiwasili kuzindua na kukabidhi nyumba hizo.
Picha ya pamoja ikipigwa na wananchi ambao wamekabidhiwa nyumba yao kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude na (kushoto) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipiga picha ya pamoja na akina Mama ambao wamekabidhiwa nyumba zao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464