SHEREHE ZA POLISI FAMILY DAY SHINYANGA ZAFANA,ASKARI WATUNUKIWA VYETI VYA PONGEZI
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limefanya Sherehe ya Polisi Family day, pamoja na kuwatunuku vyeti vya pongezi Askari ambao wamefanya vizuri kwa Mwaka 2023 katika Vikosi mbalimbali.
Sherehe hizo zimefanyika leo Februari 3,2024 katika viwanja vya Jeshi la Polisi Kambarage na kuhudhuriwa na wananchi, Falimilia za Polisi huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Mndeme akizungumza wakati wa kutoa hotuba, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kulinda usalama wa raia na mali zao na kudumisha amani, huku akiwataka kikosi cha usalama barabarani kuongeza kasi ya kudhibiti ajali, na kutokuwa na huruma na madereva ambao wanakiuka Sheria za barabarani.
"Nawapongeza Askari ambao leo mmetunukiwa vyeti kutokana na kazi nzuri ambayo mmeifanya mwaka uliopita endeleeni na juhudi hizo kwa mwaka huu, pamoja na Askari wengine ili Mkoa wetu uendelee kuwa salama," amesema Mndeme.
"Natoa wito kwa Askari wa kikosi cha usalama barabarani ongezeni kasi ya kusimamia Sheria za Barabara ili kudhibiti Ajali, msiwafumbie macho Madereva wasiofuata Sheria za barabarani wachukulieni hatua,"ameongeza Mndeme.
Katika hatua nyingine RC amewataka Askari kuendelea kuzuia uharifu pamoja na wapelelezi kuharakisha upelekezi ili watuhumiwa wafikishwe Mahakamani na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Pia ametoa wito kwa wananchi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uharifu ili wahusika wakamatwe na Mkoa kuendelea kuwa salama.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amesema wamefanya Sherehe hizo za Polisi Family day, kwamba kipindi cha Sikukuu za Kitaifa ikiwamo Christmas na Mwaka mpya, Askari hao walikuwa kazini kuhakikisha Amani inatawala ndipo wakaona ni vyema na wao kufurahi na familia zao, na kuwapongeza waliofanya vizuri mwaka uliopita.
Akitoa hali ya usalama, amesema mkoa wa Shinyanga upo salama na Matukio makubwa ya Uhalifu ya Kijamii yamepungua,na kuahidi kwamba kwa Mwaka huu wamejipanga vyema kuhakikisha Amani inatawala mkoani humo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye sherehe hizo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye Sherehe hizo.
Viongozi wakiwa Meza kuu.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Askari Polisi wakiwa kwenye Sherehe yao Polisi Family Day.
Askari Polisi wakiendelea na Sherehe.
Askari Polisi wakiendelea na Sherehe.
Askari Polisi wakiendelea na Sherehe.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa vyeti vya Pongezi kwa Askari waliofanya Vizuri mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kutoa vyeti vya pongezi.

Askari Polisi waliopewa vyeti vya pongezi.
Msanii Oscar Nyerere akitoa burudani kwa kuigilizia sauti ya Hayati Mwalimu Nyerere.
Maonesha ya Mbwa yakiendelea kwenye Sherehe hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akicheza na Jeshi la Jadi Sungusungu wakiwa wakitoa burudani kwenye sherehe hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akicheza na Jeshi la Jadi Sungusungu wakiwa wakitoa burudani kwenye sherehe hizo.
Burudani ikiendelea kutolewa kwenye sherehe hizo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464