RUWASA SHINYANGA WASAINI MIKATABA 7 NA WAKANDARASI UJENZI MIRADI YA MAJI

RUWASA SHINYANGA WASAINI MIKATABA 7 NA WAKANDARASI UJENZI MIRADI YA MAJI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAKALA wa Majisafi na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)mkoani Shinyanga, wamesaini Mikataba 7 ya ujenzi wa Miradi ya maji na Wakandarasi yenye thamani ya Sh.bilioni 6.4 itakayo tekelezwa katika wilaya ya Kahama, Kishapu na Shinyanga.
Hafla ya Utiaji saini Mikataba hiyo imefanyika leo Februari 5, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme.

Mndeme akizungumza kwenye hafla hiyo ya utiaji saini mikataba ya ujenzi miradi ya maji, amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha nyingi mkoani humo na kutekelezwa miradi ya maji, na kuondoa kero kwa wananchi pamoja na kumtua ndoo kichwani Mwanamke.
Amesema ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia Mkoa huo wa Shinyanga katika Sekta ya Maji pekee wameshapokea kiasi cha fedha Sh.bilioni 541, na kwamba leo tena ameshuhudia Utiaji Saini Mikataba 7 ya ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya Sh.bilioni 6.4, itakayo tekelezwa katika wilaya ya Kishapu, Shinyanga na Kahama na kuhudumia vijiji 17.

Aidha, amewataka Wakandarasi ambao wamesaini Mikataba hiyo ya ujenzi wa Miradi ya Maji, kwamba waitekeleze kwa kiwango kinachotakiwa na thamani ya fedha ionekane (Value For Money) pamoja na kuikamilisha kwa wakati.
“Wakandarasi kaitekelezeni Miradi hii kwa ubora unaotakiwa na thamani ya fedha ionekane, na mnunue maungio mazuri kwa ajili ya kuzuia mivujo ya maji, na miradi hii tunataka iwe endelevu kwa kizazi cha sasa nacha baadae, kuweni Wazalendo na nchi yenu zingatieni na ubora wa mabomba yasiwe yanapasuka pasuka,”amesema Mndeme.

Ametaja hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa katika maeneo ya vijijini mkoani Shinyanga kuwa ni asilimia 66 kutoka asilimia 60, na kwamba hadi kufikia mwaka 2025 upatikanaji wa maji vijijini utakuwa asilimia 85.
Katika hatua nyingine, amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuitunza miundombinu ya miradi ya maji, pamoja na kutumia maji safi na salama ambayo yanatekelezwa kwenye miradi, na kuacha kutumia maji ya kwenye Mito na Mabwawa.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amempongeza Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi ya maji mkoani humo na kumtua ndoo kichwani mwanamke, huku akiwataka Wakandarasi waitekeleze miradi hiyo ya maji kwa ufanisi mkubwa.
Amempongeza pia Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, kwa Moyo wa uzalendo na kumsaidia Rais Samia katika utekelezaji Mkubwa wa Miradi ya Maji mkoani humo.

Meneja Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, amesema, wamesaini Mikataba Saba ya ujenzi wa miradi ya Maji kutoka kwa Wakandarasi yenye thamani ya Sh.bilioni 6.4 ambayo itatekelezwa katika vijiji 17 kutoka Wilaya ya Shinyanga, Kahama na Kishapu.
Amesema Miradi Sita itahusika kwenye ujenzi wa miradi ya maji, na mradi mmoja ununuzi wa bomba pamoja na viungio na kwamba miradi yote inatarajiwa kukamilika ndani ya siku 45 hadi 360.

Naye Mmoja wa Wakandarasi Stephen Owawa kutoka Kampuni ya Geo Statia Classic Works Ltd, akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi wote ambao wamesaini Mikataba ya Maji, amesema hawataiangusha Serikali bali wataitekeleza miradi hiyo kwa ubora zaidi na kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini Mikataba 7 ya ujenzi Miradi ya Maji.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akizungumza kwenye Utiaji Saini Mikataba 7 ya Ujenzi Miradi ya Maji.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye Utiaji Saini Mikataba 7 ya Ujenzi wa Miradi ya Maji.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye hafla ya Utiaji Sain Mikataba 7 ya Ujenzi Miradi ya Maji.
Meneja RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akitoa taarifa ya Utiaji Saini Mikataba 7 ya Ujenzi wa Miradi ya Maji.
Zoezi la Utiaji Saini Mikataba ya Ujenzi Miradi ya Maji likiendelea kati ya RUWASA na Wakandarasi.

Wakandarasi waliosaini Mikataba Ujenzi Miradi ya Maji wakipiga picha ya pamoja na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela (wakwanza kushoto).
Viongozi wakiwa meza kuu.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia zoezi la Utiaji Saini Mikataba 7 ya Ujenzi Miradi ya Maji.
Viongozi mbalimbali wakiendelea kushuhudia zoezi la Utiaji Saini Mikataba 7 ya Ujenzi Miradi ya Maji.

Zoezi la ushuhudiaji Mikataba 7 ya Ujenzi wa Miradi ya Maji likiendelea.
Viongozi mbalimbali wakiendelea kushuhudia zoezi la Utiaji Saini Mikataba 7 ya Ujenzi Miradi ya Maji.
Awali Wakandarasi wakisikiliza Nasaha za viongozi mbalimbali kabla ya kusaini Mikatabaya Ujenzi Miradi ya Maji.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464