WAZAZI MTOTO ALIYEDAIWA KUZAMA MTO MHUMBU WAOMBEWA DUA,MSIBA WASITISHWA MWILI WA MTOTO BADO HAUJAPATIKANA

Maombi ya Dua.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZAZI na Familia ya Mtoto Salumu Matheo (11) Wakazi wa Mtaa wa Mbuyuni Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wameombewa Dua ili Mwenyezi Mungu awape subila kwa tukio hilo la kumpoteza Mtoto wao, ambaye hadi sasa Siku ya Nane bado hajapatikana tangu alipodaiwa kuzama ndani ya Maji Mto Mhumbu.
Dua hiyo imefanyika nyumbani kwa familia ya Mtoto huyo, ikiongozwa na Sheikh Hamis Nkingo wa Msikiti wa AQSWA, ikiwa ni sehemu pia ya kusitisha Msiba wa Mtoto huyo,mara baada ya mwili wake kutopatikana ndani ya maji katika Mto Mhumbu alipozama.

Sheikh Nkingo amesema, wamefanya dua hiyo kwa ajili ya kuwaombea wazazi wake na familia ya Mtoto huyo aliyepotea, ili Mwenyezi Mungu awape faraja kwa tukio hilo.
“Tupo hapa kwa ajili ya kufanya Dua kuwaombea wazazi wa Mtoto aliyepotea ili Mwenyezi Mungu awape subila kwa hili,”amesema Sheikh Nkingo.

Aidha, amesema kwa taratibu za kidini licha ya kusitisha msiba huo, kwamba siku kiungo chochote cha Mtoto huyo kikipatikana kitafanyiwa taratibu zote za mazishi kwa kuwakilisha mwili mzima kwa kuzingatia mambo Manne ikiwamo kuoshwa, kuvikwa Sanda, kuombewa na kuzikwa kwenye makazi yake ya milele.
Naye Baba Mzazi wa Mtoto huyo Matheo Peter, akizungumza jana wakati wa kuhitimisha msiba huo, amesema jitihada za kuupata mwili wa mtoto wake zimeshindikana.

“Tangu siku ya tukio Februari 4 tulitangaza msiba, familia, ndugu jamaa,marafiki na wananchi wamekuwa wakija kuomboleza nasisi wakati tukiendelea kuutafuta mwili wa mtoto wangu ndani ya maji, lakini hakuna mafanikio ndipo tukaona tusitisha msiba hadi pale mwili wake utapopatikana,”amesema Matheo.
Aidha, amesema kwa sasa wanamwachia mwenyezi Mungu, huku akitoa shukrani kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi, kwa jitihada zao walizozifanya za kuutafuta mwili wa mtoto wake ndani ya maji licha ya kutofanikiwa kuupata.

Bibi wa Mtoto huyo Mariamu Juma, alionyesha kuhudhunishwa na kifo cha Mjukuu wake, na kueleza kwamba siku ya tukio alikuwa amemuandalia chakula na alikula lakini hakuna maliza mara baada ya kupitiwa na marafiki zake, na lipomtafuta ili amalizie chakula hakumuona tena hadi kuja kupewa taarifa kwamba amezama Mtoni.
Amesema kilichotokea wanamuachia Mungu kwa mapenzi yake, na kutoa wito kwa wananchi ambao wapo jirani na Mto huo, kwamba siku wakiona mwili wa mjukuu wake watoe taarifa kwa viongozi wa maeneo yao ili zipate kuwafikia na kufamfanyia mazishi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukaleli Kata ya Ndembezi Japhet Kisusi ambaye Mto Mhumbu upo kwenye eneo lake, amesema tayari alikwisha wasiliana na viongozi wenzake ambao wapo pembezoni na Mto huo, kwamba siku wakisikia kuna mwili wowote umeonekana wampatie taarifa.
Tukio la Mtoto Salumu Matheo (11) kudaiwa kuzama ndani ya maji Mto Mhumbu lilitokea Februari 4 mwaka huu Majira ya Saa 12 jioni, wakati alipokwenda na wenzake watatu kuvua Samaki katika Mto Mhumbu na kisha kuanza kuogelea ndipo akazama.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Maombi ya Dua yakiendelea.
Maombi ya Dua yakiendelea.
Maombi ya Dua yakiendelea.
Maombi ya Dua yakiendelea kwenye Familia ya Mtoto huyo.
Maombi ya Dua yakiendelea kwenye Familia ya Mtoto huyo.
Maombi ya Dua yakiendelea kwenye Familia ya Mtoto huyo.
Maombi ya Dua yakiendelea kwenye Familia ya Mtoto huyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464