NBS IMETOA MAFUNZO YA USAMBAZAJI NA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 WILAYANI KISHAPU

NBS IMETOA MAFUNZO YA USAMBAZAJI NA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 WILAYANI KISHAPU

Na Marco Maduhu,KISHAPU

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS)imetoa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022, kwa viongozi na Makundi Mbalimbali katika Jamii wilayani Kishapu, ili kuwajengea uwezo wa kutafsiri, kuchambua na kuyatumia matokeo ya Sensa katika kupanga,kutekeleza,kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa Sera na Mipango ya muda mfupi,wa Kati na Mrefu kwa Maendeleo endelevu.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Februari 13,2024 wilayani Kishapu ambayo yameshirikisha Viongozi wa Dini, Madiwani, Watendaji wa Vijiji,Kata,Maafisa Tarafa,Wakuu wa Idara na Makundi Mbalimbali ya Kijamii wakiwamo watu wenye ulemavu.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkunde ambaye alikuwa Mgeni rasmi, akizungumza kwenye ufunguzi wa Mafunzo hayo, amewasisitiza viongozi na watendaji wote, kwamba matokeo hayo ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022, pamoja na Takwimu nyingine za Kisekta zilizowasilishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kuwa ndiyo ziwe msingi wa kufanya Maamuzi ya Maendeleo katika wilaya ya Kishapu.
“Matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka (2022), Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi, yawe ndiyo dira yetu inayotuongoza katika kuandaa na kuhuisha Sera, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa Mipango na Program za Maendeleo ya Mkoa na wilaya yetu ya Kishapu na kutathimini utekelezaji wake,”amesema Mkude.

“Katika upangaji wa Mipango yetu haina budi kuzingatia Matokeo ya Viashiria mbalimbali vya Matokeo ya Sensa, na zaidi tuzingatie Mwenendo wa kasi ya ongezeko la Idadi ya watu wilayani Kishapu,”ameongeza Mkude.
Aidha, amesema baada ya mafunzo hayo Matarajio ni kuona Mipango mizuri itakayotoa majibu ya Changamoto mbalimbali za Maendeleo zinazowakabili wananchi, hususani Mipango inayojieleza katika kuondoa umaskini wakipato, na hatimaye kuinua kiwango cha hali ya Maisha kama inavyoelekezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.

“Kama mnavyofahamu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekamilisha na kuzindua Ripoti mbalimbali za Sensa, Ripoti hizi zimebainisha hali ilivyo katika Sekta mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya hadi Kata, Matumizi haya Matokeo ya Sensa yatatusaidia kufahamu tupo wangapi katika maeneo yetu kwa jinsi,umri, na fursa za kiuchumi zilizopo pamoja na taarifa nyingine za kidemografia,
“Matokeo haya ya Sensa yanabainisha pia hali halisi ya upatikanaji wa ubora wa huduma za kijamii, kama Maji, Miundombinu ya Barabara, Afya, Elimu, Nishati, Masoko, Mabenki na Mawasiliano, hivyo Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ni nyenzo Muhimu ya Kisera katika utekelezaji wa Majukumu yetu kwa ufanisi, na hatuna budi kuyaelewa na kufahamu matumizi yake kwani ni Jambo la Msingi ambalo litachochea kasi ya kutatua kero za Wananchi na kuwaletea Maendeleo kwa usawa,”ameeleza Mkude.

Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), amesema wametoa Mafunzo ambayo yanatolewa nchi nzima, kwamba lengo lake ni kuwajengea uelewa viongozi mbalimbali na makundi juu ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 katika Uandaaji na utekelezaji wa Program za Maendeleo.
Aidha, ameshauri Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa Makundi Mbalimbali katika Jamii kwamba pindi wanapohitaji Takwimu za Sensa kwenye maeneo yao waombe taarifa kwenye Ofisi za NBS pamoja na kutembelea Tovuti ya NBS.

"Tunajua mna mahitaji mengi kwenye matokeo haya ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, tunaomba kama kuna mahitaji ya takwimu, tuandikieni barua kwenye Ofisi za mkoa, tutawapatia takwimu mnazohitaji pamoja na kutembelea Tovuti za NBS",amesema Mugambi.
Mtakwimu Mwinyi Omary kutoka NBS akiwasilisha taarifa za usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022, amesema Tanzania kwa sasa ina idadi ya watu Milioni 61.7, ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga wapo Milioni 2.2, na wilaya ya Shinyanga ni 468.661, Kahama Manispaa 453,654, Ushetu 390,593, Msalala 378,214, Kishapu 335,483 na Manispaa Shinyanga Idadi ya watu ni 214,744.

Kauli Mbiu ya Matokeo ya Sensa ya Sita inasema “Mipango Jumuishi kwa Maendeleo Endelevu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye Mafunzo hayo ya NBS.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye Mafunzo hayo ya NBS.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye Mafunzo hayo ya NBS.
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka NBS. Benedict Mugambi akizungumza wakati wa utoaji wa mafunzo hayo.
Mtakwimu kutoka NBS Mwinyi Omary akitoa Mafunzo.
Mtakwimu kutoka NBS Rahimu Daudi akitoa Mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye Mafunzo ya NBS.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo kutoka NBS.
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka NBS. Benedict Mugambi wapili kulia, akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude Ramani ya Sensa ya watu na Makazi ya wilaya hiyo.
Zoezi la Makabidhiano ya Ramani ya Sensa ya watu na Makazi likiendelea.
Zoezi la Makabidhiano ya Ramani ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Kata likiendelea.
Zoezi la Makabidhiano ya Ramani ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Kata likiendelea.
Zoezi la Makabidhiano ya Ramani ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Kata likiendelea.
Zoezi la Makabidhiano ya Ramani ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Kata likiendelea.
Zoezi la Makabidhiano ya Ramani ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Kata likiendelea.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464