RC Mndene alimulika Bwawa la Songwa kueneza Kipindupindu Shinyanga
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Chistina Mndeme,amewataka wadau wa Maji mkoani humo na Mamlaka zinazohusika kushirikiana na Maafisa Afya Kutibu Maji katika Bwawa la Songwa lililopo wilayani Kishapu,ambalo kwa sasa linadaiwa kuwa ndiyo Chanzo cha kueneza Ugonjwa wa Kipindupindu.
Mndeme amebainisha hayo leo Februari 14,2024 wakati akifungua kikao cha Kamati ya huduma za Afya ya Msingi kwa ajili ya Maandalizi ya Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo dhidi ya Magonjwa ya Surua na Rubella, Tathimini ya Lishe na Mwenendo wa Ugonjwa wa Kipindupindu.
Amesema katika Mkoa wa Shinyanga tangu Disemba 2023 hadi Februari 12 mwaka huu, kuna Wagonjwa wa Kipindi pindu 192, ambapo Kishapu wapo 109, Kahama 60, Manispaa ya Shinyanga 23 huku Vifo vikiwa Sita, na kwamba Februari 13 kumeibuka wagonjwa wapya 11 ambao wanatoka wilayani Kishapu Kata ya Maganzo,Songwa na Mwigumbi Chanzo kikiwa ni Maji ya Bwawa la Songwa.
“Haiwezekani Ugonjwa huu wa Kipindupindu ulikuwa umesimama lakini umeibuka upya ukitokea Maganzo, Songwa, na Mwigumbi na Chanzo kikiwa ni Bwawa la Maji la Songwa Mamlaka zinazohusika na bwawa hilo kwa kushirikiana na Maafisa Afya kayatibuni maji hayo ili kuzuia kuenea kwa Ugonjwa huu wa Kipindupindu,”amesema Mndeme.
Aidha, Mndeme ametoa Rai kwa wananchi wa Mkoa huo kwamba katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa Kipindupindu, watumie Maji yaliyochemshwa au kutibiwa kwa vidonge vya Klorini, kutumia vyoo bora, pamoja na wadau wa Maji kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwenye maeneo yenye changamoto.
Naye Dk. Magenda Kihulya kutoka (TAMISEM) amesema Ugonjwa wa Kipindupindu ni aibu, na hivyo kuwasihi Wananchi wazingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya pamoja na kuwa na vyoo bora, na kwamba Sheria inasema watu wasio na vyoo wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu, amesema katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa Kipindipindu, kwamba Mkoa umejipanga kuendelea kutekeleza njia mbalimbali za udhibiti ugonjwa huo ili usiweze kuenea, kwa kugawa dawa za kinga za kutibu Maji( Aqua Tab) na kufanya ukaguzi wa Kaya zisizo na vyoo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu RMO Mkoa wa Shinyanga Fuastine Mlyutu akizungumza kwenye kikao hicho.
Dk.Mageda Kihulya kutoka TAMISEM akizungumza kwenye kikao hicho.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Muonekano wa baadhi ya maeneo bwawa la Songwa.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiendelea na kikao.
Kikao kikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464